KITAIFA

KIHENZILE AITAKA LATRA KUDHIBITI MADEREVA WANAOCHEZEA MFUMO WA VTS

KIHENZILE AITAKA LATRA KUDHIBITI MADEREVA WANAOCHEZEA MFUMO WA VTS

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameutaka Uongozi Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kukahikisha ianwachukulia hatua za kisheria Madereva wote wanochezea Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) .


Kihenzile meyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea ofisi ya LATRA Mkoa wa Dar es Salaam Mtaa wa Nkrumah na kituoa cha Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) kilichopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ikiwemo idara ya utoaji leseni za vyombo vya moto kibiashara na idara ya usajili na uthibitishaji wa madereva wa vyombo hivyo.


“ Nimepewa taarifa kuwa kunabaadhi ya Madereva wanachezea Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS ) hii ni hatari hivyo nawaelekeza uongozi wa LATRA kuhakikisha wanawdhibiti Madereva hao ili wasije wakasababisha ajari”. Amesema Mhe. Kihenzile.


Kwa upande wake Prof. Ahmed Mohamed Ame, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi LATRA amesema kuwa LATRA inaendelea kuboresha Mfumo wa VTS hadi kufikia kutoa namba ya malipo (control number) moja kwa moja pale dereva napokiuka Sheria za Usalama Barabarani pamoja na kuongeza kasi ya kudhibiti mabasi yanayofanya safari za saa 24.


“Tunaedelea kukaa na wenzetu Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ili tuweze kufanya mambo mengi kwa pamoja hadi kufikia Mfumo kuweze kutuma namba ya malipo moja kwa moja kwa kutoa adhabu pindi dereva anapokiuka Sheria za barabarani ili tuweze kudhibiti mabasi yanayofanya safari za usiku kama tulivyo agizwa na Wizara” Amesema Prof. Ame.


Naye Bw. Johansen Kahatano, Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara amesema, hadi sasa madereva 2757 wameshafanya mtihani wa kuthibitishwa na LATRA na madereva 1817 wamefaulu na wengine kuendelea kurudia mtihani huo. Na tumeona madereva wengi wanaothibitishwa wamekuwa wakizingatia Sheria na wanaendelea kufuatiliwa mienendo yao wawapo barabarani.


“Inatupa faraja kuona kwamba tangu mwezi Septemba hadi sasa madereva tuliowathibitisha kwa kuwapatia mtihani na kufaulu hawajasababisha ajali za barabarani zinazo athiri binadamu na mali zao na tunaendelea kuwafuatilia kwa ukaribu zaidi wale madereva wavunjifu wa Sheria hususana wanaochezea Mfumo wa VTS na hatutosita kuwachukulia hatua za Kisheria” Ameeleza Bw. Kahatano.


Mamalaka inaendelea kuboresha huduma katika sekta ya Usafiri Ardhini kwani ni sekta bora na inahakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi yetu.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *