BIASHARA

SHILINGI BILIONI 75.8 KUGHARAMIA UJENZI BANDARI YA MBAMBA BAY NYASA RUVUMA.

SHILINGI BILIONI 75.8 KUGHARAMIA UJENZI BANDARI YA MBAMBA BAY NYASA RUVUMA.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) imeingia mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba bay iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, mradi utakao gharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.8 ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24.


Akizungumza na wananchi katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Waziri wa Uchukuzi Prof. makame Mbarawa amesema ujenzi wa bandari hiyo unaofanywa na kampuni ya Xiamen-ongo,ng Construction Limited kutoka nchini China utakapokamilika utatoa fursa ya usafirishaji katika ushoroba wa Tanzania na Zambia pia sekta binafsi na watu wengine hivyo kuongeza fursa za ajira na kuinua uchumi.


“Utekelezaji wa mradi huu ni hatua kubwa katika historia ya nchi yetu ambao umefanywa na serikali ya awamu ya sita, utakumbuka wiki iliyopita mikataba miwili imesainiwa kati ya Tanzania na Malawi nia ni kuongeza ufanisi wa usafirishaji kwenye ziwa hili (Nyasa),” Amesema Waziri Mbarawa.


Aidha Prof. Mbarawa amemuagiza mkandarasi kuhakikisha wakazi na wananchi wa wilaya ya Nyasa kuwa wanufaika wa kwanza wa nafasi mbalimbali za ajira zitakazotokana na ujenzi wa bandari hiyo huku akiiagoza TPA kulisimamia jambo hilo.


Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce Mbossa amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 bandari ya Mbamba bay ilikusanya shehena kubwa Zaidi kulinganisha na bandari zote katika ziwa Nyasa, jambo lililosababisha kufikiwa kwa maamuzi ya Mbamba bay kuwa makao makuu ya bandari zote katika ziwa hilo.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameishukuru sana serikali kwa mradi huo huku akisema huo ni mradi wa kwanza katika wilaya hiyo kuwa wenye gharama kubwa Zaidi jambo linaloonyesha namna serikali inavyowajali wananchi wa eneo hilo.

About Author

Bongo News

3 Comments

    2003; 21 341 345 best site to buy priligy ATN typically affects both kidneys and has a multifaceted etiology that includes ischemic injury, contrast material induced nephropathy, and nephrotoxic effects of drug therapy

    All views are those of UKMCCS priligy online

    Category Steroids cytotec price uae Refined molecular subtyping and recognition of key genetic mechanisms constitutes an encouraging basis for further development of subtype specific targeted therapies

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *