KITAIFA

MAKONDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

MAKONDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUDUMISHA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

Awaomba kuendela kutoa ushauri mzuri na kutoa miongozi itakayowasaidia Viongozi wa Chama na Serikali kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa misingi ya Haki.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Paul Christian Makonda, amewashukuru na kuwaomba Viongozi wote wa Dini nchini, kudumisha ushirikiano kwa viongozi wa Chama na Serikali, kwa kushauri na kutoa miongozo itakayowasaidia kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa haki na ufanisi ili kugusa matumaini yao kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo nchini.

Mwenezi Makonda amesema hayo alipokwenda kumuona na kumsalimia Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Baba Askofu Flavian Matindi Kassala , ofisini kwake, jimboni, mtaa wa Kambarage 14, mjini Geita, leo Alhamis, Disemba 28, 2023, ukiwa ni mwendelezo wa utaratibu wale wa kwenda kuwaomba ushirikiano, ushauri na miongozo mbalimbali viongozi wa kiroho wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini, pamoja na makundi mengine ya kijamii, utakaomsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa upande wake, Mhashamu Baba Askofu Kassala, pamoja na kumtakia kila la heri, amemhakikishia Mwenezi Makonda kuwa viongozi wa Dini wataendelea kutoa ushirikiano wao katika kuiombea Nchi, kuwashauri Viongozi na kuwapatia miongozo mbalimbali itakayowasaidia kuendelea kuwa watumishi bora wa wananchi, wanapotekeleza majukumu yao ya kuiongoza nchi kwa haki na upendo ili pia kudumisha umoja na mshikamano Kiongozi mwa Watanzania.

Aidha, Kwa pamoja wamefanya maombi ya kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kuwa na Afya njema ili kuendelea kulitumikia Taifa letu la Tanzania.

Huu ni muendelezo wa Ziara za Mwenezi Makonda katika kuwatembelea Viongozi mbalimbali wa Dini Nchini.

About Author

Bongo News

1 Comment

    In a similar way, our results may indicate a modest improvement in HPA axis regulation in the intervention group but further research is needed to confirm this and delineate the precise determinants of HPA axis modulation buy priligy tablets Capsules; Oral; Doxycycline Hyclate 100 mg Tablets, Film Coated; Oral; Doxycycline Hyclate 100 mg

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *