Matukio mbalimbali katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kilichotanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa.
Vikao hivyo vimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia Vikao hivyo, Wajumbe wa Halamshauri Kuu kwa sauti moja wameridhia Ndugu. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa na kumpokea kwa Furaha, Upendo na Bashasha.
Naye, Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi ametanguliza shukrani zake za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini na kumpotisha kuwa katika kuhudumu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – Taifa.