KITAIFA

MAJANGA MINDU, WANANCHI WAVAMIA MLIMA WAJENGA KANDO YA MTO, MECIRA WAFIKA KWENYE ENEO WAPAZA SAUTI

MAJANGA MINDU, WANANCHI WAVAMIA MLIMA WAJENGA KANDO YA MTO, MECIRA WAFIKA KWENYE ENEO WAPAZA SAUTI

• Maafa yaliyotokea Hanang kwa waliojenga njia ya maji yanaweza kutokea Morogoro wakati wowote kutoka sasa baada ya uvamizi kuzunguka hifadhi yam lima mindu kushika kasi

•Wananchi wajenga nyumba kandoni mwa mto Mindu, waanzisha mashamba bila kuzingatia kanuni inayokataza shughuli hizo ndani ya mita 60

•Makorongo yanayotiririsha maji na mawe Yazidi kuongezeka chini ya mlima unaohifadhiwa

• Mlaji yanayotoka mlima Mindu ni moja kati ya vyanzo muhimu vya maji yanayonywewa na wakazi wa mji wa Morogoro baada ya kuchakatwa bwawa la Mindu

• PAZA SAUTI ya MECIRA yatia kambi kujionea, yapongeza jitihada za TFS kunusuru hifadhi ya msitu huo

Mwandishi wetu,

Miezi michache baada ya Taifa kushuhudia maafa yaliyotokana na maporomoko ya matope, maji, magogo na mawe yaliyoathiri na kuchukua Maisha ya watanzania kadhaa wakazi katesh wilayani Hanang mkoani Manyara, hali kama au zaidi ya hiyo inaweza kutokea kwa mamia ya wakazi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi yam lima mindu uliopo Morogoro baada ya uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa katika eneo hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi wa Morogoro kiasi cha kusababisha makorongo makubwa yanayopitisha maji kutoka mlima Mindu kupeleka mto mindu na baadae bwawa la Mindum aji ambayo huchakatwa pia kwa matumizi ya binaadamu mkoani humo

BONGONEWS  imeshuhudia jambo hili katika ziara maalum ya kujielimisha iliyoandaliwa na taasisi ya Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (MECIRA) kwenye mradi wao wa PAZA SAUTI, jitihada za dharura zinahitajika kuunusuru mlima huo ambao unazii kuathiriwa kwa kuvamiwa na wananchi wanaoanzisha makazi siku hadi siku huku shughuli za kibinaadam ikiwemo ukataji miti na uchimbaji michanga zikitishia sio tu usalama wa hifadhi ya mlima huo bali hata Maisha ya wakazi wenyewe wa vijiji vinavyouzunguka mlima mindu

Taarifa zinasema kuwa eneo hilo awali lilikuwa si la makazi ya binadamu, bali kwa sasa binadamu wamevamia, hivyo shughuli za ujenzi, uvunaji wa mchanga, ukataji wa miti na ufugaji kando ya mlima huo, zimeendelea kulifanya kuwa hatarishi Zaidi.

Pamoja na wananchi kujenga kandoni mwa makorongo makubwa yam aji, hali yam to mindu unaotegemewa kupeleka maji bwawa la mindu pia iko hatarini baada ya wakazi kujenga nyumba na kuendeleza mashamba ya mazao mbalimbali mita chache pembezoni mwa mto huo bila kuzingatia sheria zinazowataka wananchi kufanya shughuli za kibinadamu umbali wa mita 60 kutoka katika chanzo cha maji ikiwemo mito, milima, ardhioevu na misitu

Elizaberth Magambo ni mama ambaye amejenga nyumba yake mita tatu tu kutoka usawa wa korongo kubwa linalopitisha maji kutoka mlima mindu ambalo linazidi kuongezeka ukubwa kila mvua zinaponyesha anasema yupo katika hatari na anaiomba Serikali iweze kuwapatia ardhi katika maeneo mengine

“Tupo katika wakati mgumu, tulijua kuwa hii ni kanani yetu lakini imekuwa tofauti, tunatamani kuhama hata kesho ila hatuna uwezo, usiku hatulali hasa kipindi hiki cha mvua, tunaiomba Serikali iingilie kati na kutunusuru kabla mambo hayajaharibika” alisema

Alisema walipohamia eneo hilo halikuwa na makorongo makubwa bali shughuli za binadamu kama vile kuchimba mchanga kwa ajili ya kuuza, ndiyo chanzo kikubwa cha kuharibika kwa eneo hilo.

Uchunguzi wa Mecira umebainisha kuwa pamoja na wakazi wa eneo hilo kuwa karibu kabisa na mlima Mindu hicho kwao si kikwazo kwani nyumba zinaendelea kujengwa kwa kasi.

Aidha uchunguzi huo umebaini pia kuwa asilimia kubwa ya wananchi waliojenga nyumba katika mazingira hayo waliyavamia wakijua kuwa ni sehemu salama ya makazi lakini sasa imekuwa ni majuto kwani nyumba zao zipo katika hatari ya kumezwa na makorongo hayo yanayoendelea kutanuka siku kwa siku.

Kama hiyo haitoshi Mecira ilikutana na jamii ya kabila la wamasai ambao wanachunga ng’ombe katika mlima huo wa Mindu,walipoulizwa kuwa kwa nini wanalisha mifugo yao kwenye hifadhi ya mlima huo walibainisha kuwa wapo katika eneo hilo kwa muda sasa na wameshayaozea maisha hayo.

Shughuli za kilimo, ukataji wa miti, ujenzi holela na uchimbaji wa mchanga vimetajwa kuwa vyanzo vikubwa vya uharibifu na uchafuzi wa mazingira katika eneo hilo la Mindu.

Ili bwawa la Mindu liendelee kupokea maji na kuwasaidia wananchi wa morogoro, mlima mindu unatakiwa kutunzwa na kuhifadhiwa kwa wivu mkubwa kwa madhumuni ya kuendelea kutiririsha maji yake katika mto Mindu na maji hayo kwenda moja kwa moja katika bwawa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *