Mhe. Mkuu wa Mkoa Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Mei 16 wakati alipokuwa akikabidhiwa pikipiki 20 kwaajili ya kuimarisha Ulinzi na usalama Mkoani Arusha, pikipiki ambazo zimetolewa na Benki ya Biashara ya CRDB ikiwa ni sehemu ya programu yake ya kurudisha kwenye Jamii.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema miongoni mwa ahadi zake ilikuwa ni pamoja na kuliimarisha Jeshi la Polisi kwa kuwapatia Nyenzo za ufanyaji wa kazi katika kuimarisha Ulinzi na usalama Mkoani Arusha ambapo aliahidi kuwatafutia pikipiki 50, Baiskeli za Umeme 100 na magari 20 kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Mhe. Makonda amesema anatambua kuwa Usalama ni kivutio namba moja katika kuvutia utalii Mkoani Arusha na hivyo ameishukuru Benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maagizo yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kuhakikisha anakuza utalii kwenye mkoa wa Arusha.
Mhe. Mkuu wa mkoa pia amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kuendelea kuwekeza Mkoani Arusha na anasema kufikia Mwezi Julai tarehe 30 Biashara ndani ya Mkoa wa Arusha zitakuwa zinafanyika kwa saa 24 kwani Usalama na Ulinzi wa mkoa utakuwa umeimarika kwa kiwango cha juu kabisa.
Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuomba Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela kuandaa Mpango maalumu wa usaidizi wa mikopo kwa wawekezaji wa ndani, ili kuwezesha Ujenzi wa Malazi ya kutosha Mkoani Arusha katika jitihada za kuondoa ufinyu wa nyumba za kulala wageni na watalii wanaofika mkoani Arusha kutalii na kwenye mikutano na warsha mbalimbali.
Mhe. Mkuu wa Mkoa pia amevishukuru vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani Arusha kwa kuendelea kupunguza uhalifu kwa kasi kubwa akihaidi kuendelea kushirikiana nao katika kuwawezesha vitendea kazi na dhana mbalimbali ili kuondosha vikwazo katika majukumu yao.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ameahidi kuyafanyia kazi maombi yote ya Mhe. Mkuu wa Mkoa na kutangaza kushirikiana naye katika programu ya Mkuu wa Mkoa ya kulifanya Jiji la Arusha kuwa safi ambapo CRDB wameahidi kutoa na kufunga vifaa vya kutunzia taka kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Aidha Nsekela katika kuendelea kuunga Mkono jitihada za Mhe. Makonda za kuimarisha Ulinzi na Usalama mkoani hapa, ameahidi kuanzisha programu maalum ya kuwaunganisha vijana wa Arusha katika Makundi mbalimbali yatakayopatiwa mikopo yenye riba nafuu na elimu mbalimbaki za ujasiriamali ili waweze kuachana na uhalifu na kujikita katika uzalishaji mali.
Benki ya CRDB ipo mkoani Arusha ambapo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwenye sekta ya elimu na afya ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki hiyo unaotarajiwa kufanyika Ijumaa ya Mei 17, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Makabidhiano ya Pikipiki hizo yamekwenda na kaulimbiu ya CRDB isemayo “Kuimarisha usalama na Kukuza Utalii mkoani Arusha” na imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa, Maafisa mbalimbali wa Benki ya CRDB Taifa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha.
2 Comments
Excellent site. Plenty of helpful information here. I’m sending it to some buddies ans additionally sharing in delicious. And naturally, thanks for your sweat!
Международная логистика играет центральное значение в налаживании цепочек поставок в регион. Это комплексный подход, включающий транспортировку, обработку документов и оптимизацию логистики. Точное управление и выбор надежных партнеров минимизируют риски и гарантируют своевременную доставку.
Одной из важнейших целей в ввозе товаров является определение маршрута – https://ved-mezhdunarodnaya-logistika.ru/ . Для организации поставок используются комбинированные решения: морские перевозки экономически эффективны, авиатранспортировка — для скоропортящихся, а наземный транспорт — для баланса скорости и цены. Географическое расположение нередко требует комбинированные маршруты.
Не менее ключевой частью является оформление документов. Компетентное оформление таможенным бумагам, соблюдение стандартов и анализ санкционного давления минимизируют проблемы. Работа с профессионалами учитывает все нюансы, что критично для результата.
Автоматизация процессов активно изменяют работу с импортом. Трекеры грузов, системы складского учета и технологии big data улучшают эффективность поставок. Бизнес-процессы теперь могут сохранять устойчивость, адаптироваться к требованиям и обеспечивать поставки.
Глобальные перевозки основана на стратегии, профессионализма и налаженных отношений. Это важный механизм, позволяющий отечественным бизнесам увеличивать эффективность и интегрироваться в мировую экономику.