KITAIFA

RC MAKONDA ATOA FARAJA KWA WANANCHI WALIOPATWA NA ATHARI ZA MAFURIKO – MANGAFI

RC MAKONDA ATOA FARAJA KWA WANANCHI WALIOPATWA NA ATHARI ZA MAFURIKO – MANGAFI

Atoa maagizo maji kutolewa eneo hilo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda , ametembelea katika maeneo yaliyopatwa na athari za mafuriko katika mtaa wa Mangafi yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.

RC Makonda amekutana wa wananchi wahanga wa maafa hayo na kutoa faraja ambapo amewaahidi kuwapatia magodoro pamoja na mahitaji ya chakula.

Akizungumza na viongozi akiwemo Mbunge , Diwani na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Karatu Mhe. Kolimba, RC Makonda amewataka kutauta namna ya kutatua tatizo hilo ambapo ameagiza shughuli ya kuyatoa maji hayo ianze mara moja.

Lazima tutafute jibu la kudumu kwakuwa itakuwa jambo la heri, zaidi ya kaya 700 na watu 2800 hawana makazi, si jambo zuri nitatafuta namna ya kusapoti viongozi wetu wa wilaya kuwapa faraja ninyi kwa niaba ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ,tuna magodoro na mahitaji ya chakula tutaleta kwa uongozi wa wilaya kuwakabidhi kwa kushirikiana na mbinge na diwani wenu .”

Tujitahidi sana kuwasikiliza viongozi wetu kwakuwa wana taarifa nyingi na nyingi zinatoka kwenu ikiwa pamoja na mazingira yapi yanafaa kwa jambo lipi kwahiyo tutakapombana kutoa maji haya tukubaliane pia kuwasikiliza wanasema lipi kwakuwa hakuna kiongozi atakayepeleka watu wake maeneo yasiyostahili “.

Tumuombe Mungu ya kwamba tumepata madhara kiasi kwa mvua za hivi karibuni hivyo atuhurumie tusipatwe na majanga haya tena, suala hili la kumuomba mumgu si la CCM wala CHADEMA ni watu wote .”

Kwa mujibu wa Diwani wa eneo hilo Mhe. Joseph amesema kuwa eneo hilo limejaa maji tangu katikati ya mwezi wa 4 mwaka huu ambapo amesema eneo hilo lilikuwa sehemu ya kupumulia bwawa la karatu na kutokana na uwepo wa makazo imepelekea maji kutuhuma hapo.

🗓️24 Mei, 2024
📍Wilayani Karatu – Arusha

ArushaNaUtalii

ArushaYaSamia

Siku6ZaMoto

KaziIendelee

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *