Uncategorized KITAIFA

RC MAKONDA APANDA MTI OFISI MPYA ZA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO AKIHIMIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA ARUSHA.

RC MAKONDA APANDA MTI OFISI MPYA ZA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO AKIHIMIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Mei 24, 2024, akiendelea na ziara yake ya Wilaya zote za Mkoa wa Arusha amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro linalojengwa Mjini Karatu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Ujenzi wa Jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Juni 2024 ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutaka kupunguzwa kwa shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi pamoja na kutekeleza dhamira ya Mamlaka hiyo ya kutaka kushirikiana na jamii na kuruhusu wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuweza kujiendeleza nje ya Hifadhi hiyo.

Wakati wa Ukaguzi wa ujenzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda alipanda mti ndani ya viunga vya Ofisi hizo za Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kuu za uhifadhi wa Mazingira pamoja na utunzaji wa mazingira na uimarisha uoto wa asili.

About Author

Bongo News

133 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *