Idara Uhamiaji Mkoa wa Arusha usiku wa kuamkia tarehe 05/07/2024 imefanikiwa kukamata raia 28 wa Ethiopia maeneo ya Uwanja wa ndege wa kisongo uliopo nje kidogo ya jiji la Arusha, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Idara ya Uhamiaji baada ya kuwakamata raia 28 wa Ethiopia. Kwa mujibu wa maelezo yao walikuwa wamepakiwa kwenye lori la mizigo ambalo lilipata ajali baada ya kugongana na gari lingine ndipo wakashuka na kujificha porini maeneo hayo.

Baada ya kupekuliwa baadhi ya raia hao walikutwa na majeraha kwenye miili yao haswa maeneo ya kichwani yaliyosababishwa na ajali hiyo.

Akithibitisha kukamatwa kwa raia hao Naibu Afisa wa Uhamiaji mkoani hapa Marakibu (SI) Dickson Mwandikile amesema waliingia nchini kinyume cha sheria na kwamba walitokea Kenya kwa lengo la kwenda Afrika ya Kusini kupitia Tanzania.

Idara ya Uhamiaji inaendelea kutafuta gari lililotimika kusafisha raia hao pamoja na wasafirishaji.

About Author

Bongo News

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *