Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.6 kuboresha huduma za afya ambapo kuna ujenzi wa majengo ya mama na mtoto, jengo la upasuaji na jengo la maabara katika hospitali ya wilaya ya kiteto iliyopo mkoani Manyara.

Dkt Mollel ameeleza hayo leo juli 6, 2024 wakati alipofanya ziara wilayani humo kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya .

Dkt.Mollel amesema kuwa serikali inaendelea kuborehsa huduma za afya ambapo mpaka sasa wilaya ya kiteto imepokea Vifaa vya shilingi milion 185 kutoka Bohari ya Dawa ( MSD) na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani humo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *