Raisa Said,Muheza

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko ameipa wiki mbili Halmashauri ya Muheza ihakikishe inapeleka Walimu wakike katika shule.ya sekondari Manofu iliyopo kitongoji cha Fanusi kata ya Kisiwani.

Wito huo ameutoa baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ayubu Juma kutoa Ombi la kutaka awasaidie kupata Walimu wakike katika shule hiyo yenye wanafunzi wakike 82 na wakiume 42.

Sekiboko ambaye amefika katika shule hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kuhamasisha uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura,Kuhamasisha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa lakini pia wananchi wajitokeze katika kugombea nafasi mabalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa utakafanyika miezi michache ijayo pamoja na kuhamasisha wanaCCM wajisali kwenye mfumo wa kidijitali .

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *