Na Fatuma Mkang’ata, SJMC Dar es Salaam
Kundi la mashabiki wa Simba Sc wakiongozana na viongozi kadhaa akiwemo afisa habari Ahmed Ally “semaji” wametua mjini Morogoro kuelekea hifadhi ya wanyama ya Mikumi kuzindua wiki ya Simba sambamba na kuutambulisha uzi mpya wa ubaya ubwela utakaotumika msimu wa 2024-2025.
Hatua hiyo itafungua rasmi uuzwaji wa jezi hizo ambazo wanasimba wengi wanazisubiri kwa hamu waweze kutinga nazo uwanjani siku ya Simba au Simba day inayotarajiwa kufanyika August 8 katika dimba la Benjamin Mkapa.
Taarifa tulizozipata hivi punde zinaelekeza kuwa wadau na wanachama wa Simba waliwasili Morogoro kwa njia ya treni ya kisasa majira ya saa 1 asubuhi kuelekea mbuga ya Mikumi kuzindua wiki ya Simba sambamba na kuutambulisha uzi mpya wa mnyama utakaotumika msimu wa 2024-2025 ambao mashabiki wengi wanausubiri kwa ajili ya kutinga nao uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Simba au “Simba day” inayotarajiwa kufanyika Agosti 3.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya stesheni ya Morogoro aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Simba mzee Hassan Dalali amesema usajili uliofanyika utairejesha ile Simba ya miaka minne iliyopita na kuwataka mashabiki wawe wavumilivu katika wakati huu ambao timu inapitia mabadiliko.
Sambamba na hayo amewaasa mashabiki wanunue tiketi kwa wingi wakaujaze uwanja siku ya Jumamosi kwenye tukio muhimu kwa wanasimba.