Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan huko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.
Rais Xi ameeleza kuwa mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, hivyo China inapenda kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa nchi mbili na urafiki wa jadi kati ya China na Tanzania uweze kuenziwa kizazi hadi kizazi.
Aidha ameongezea Kwa kumesema China inapenda kutumia Mkutano huo kama fursa ya kuhimiza maendeleo mapya katika ufufuaji wa Reli ya TAZARA, kushirikiana kuboresha mtandao wa usafiri wa reli na kuijenga Tanzania kuwa eneo la mfano la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Kwa upande wake rais Samia alieleza furaha yake ya kuja tena China baada ya mwaka 2022 na kuhudhuria mkutano wa kilele wa Beijing wa FOFAC. Amesema China ni mshirika mkubwa wa Tanzania anayetegemewa na asiyekosekana.
Aidha ameongezea Kwa kusema Chama cha Mapinduzi cha Tanzania CCM kina urafiki wa kindugu na Chama cha Kikomunisti cha China, na Tanzania inapenda kutumia vyema Chuo cha Uongozi cha Nyerere ili kuongeza mafunzo ya kujenga chama na kupanua ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali. Amesisitiza kuwa Tanzania inathamini sana pendekezo lililotolewa na Rais Xi Jinping la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na inafurahi kushuhudia ufufukaji wa Reli ya TAZARA katika ziara hii.
Katika mkutano huo, China na Tanzania zimetia saini nyaraka kadhaa za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo kama vile utandawazi wa miundombinu na biashara ya mazao ya kilimo
Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021.
Kwa Mwaka huu wa 2024 Rais Samia na Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha uhusiano wetu mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60
Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.
5 Comments
porn
I was able to find good information from your content.
I loved as much as you’ll receive carried out right here.
The sketch is attractive, your authored material stylish.
nonetheless, you command get got an impatience over that you wish be delivering the following.
unwell unquestionably come more formerly again as exactly the same nearly a lot
often inside case you shield this hike.
ミニ ラブドール30 on the dot,don’t miss the magnificent Symbio show in the Aqua City lagoon.
the weight of dogs increased with age.ラブドール 中古Desexing itself causes a significant rise in a dog’s weight,
These causes are likely parallel to the reasons spouses quiet quit their marriages.ロボット セックスIf you find yourself,