Na Mwandishi wetu Geita
Wakati Monyesho ya 7 ya teknolijia ya madini yakiendelea mkoani Geita makamapuni mbalimbali yameshiriki katika maonyesho hayo ikiwa ni makampuni yanayo sambaza bidhaa mbalimbali migodini hasa wauzaji wa Magari na Mitambo
Kwa mwaka huu kitu cha kipikee ni ushiriki wa shule binafsi katika maonyesho hayo ambayo Shule za Waja na Savannah Plain ni kutoka kanda ya ziwa zimeshiriki maonyesho hayo pamoja na shule za FEZA
Miongoni mwa huduma mbalimbali zinazofanywa katika banda la Feza Schools ni pamoja na Usahili wa wanafunzi kwa kidato cha kwanza kwa muula mpya wa masomo wa 2025
Akizungumza katika maonyesho wakati wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari mkoani Geita walipotembelewa katika banda lao kwa lengo la kujifunza Afisa Mratibu na msaili wa wanafunzi wa FEZA ,Huzaifa Sizya amesema wamejikita kutoa Elimu Bora zeye viwango vya kimataifa kwa shule zenye mtaala wa Kimataifa (Feza International) na viwango vya Kitaifa chini ya NECTA na kusisitiza Feza imekuwa ikiongoza katika matokeo ya Kidato cha 4 na 6 kwa miaka yote ikijivunia rekodi ya kutoa daraja la kwa nza kwa wanafuzi wote miaka zaidi ya kumi sasa
Pia FEZA iko mbioni kufungua shule kanda ya ziwa ili kuwaletea wananchi na wazazi huduma jirani na kuunga mkono juhudi za serikikali kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na si bora Elimu.
Pia FEZA ina mpango wa kuwasomesha Bure wanafunzi ambao wanauwezo wa kimasomo Darasani lakini kutokana na changamoto za Familia hawana uwezo wa kusomeshwa, Feza wana fadhili wanafunzi hao hasa wale wenye uwezo mkubwa katika masomo ya Sayansi ili kutengeneza Madaktari na wahandishi wa Baadae
1 Comment
Takipçi kitlesi Google SEO sayesinde online satışlarımız arttı. https://royalelektrik.com//beylikduzu-elektrikci/