Uncategorized KITAIFA

GFA VEHICLE ASSEMBLER YASHINDA TUZO ZA RAIS KWA UUNGANISHAJI WA MAGARI NCHINI YA MWAKA 2024. 

GFA VEHICLE ASSEMBLER YASHINDA TUZO ZA RAIS KWA UUNGANISHAJI WA MAGARI NCHINI YA MWAKA 2024. 

Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimeibuka mshindi kwanza kwa makampuni ya Kati nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) zilizofanyika jijini Dar es salaam
 
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hilyo Meneja mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng amesema anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi na tuzo hii ni ya 2 kwa kampuni ya GFA.
 
Nae mkurugenzi wa Masoko na Mawasilianao wa Kampuni hiyo, Salman Karmali alisema wao kama kampuni wanashukuru tuzo hiyo ni dalili mzuri kwani kiwanda hicho cha kuunganisha magari nchini Ndio kiwanda cha kwanza  hapa Tanzania kunganisha magari makubwa  pia tunajivunia  kuwa waongoza njia katika sekta ya Usafirishaji.
 
Pia Karmali alisema GFA ni kiwanda kikubwa kilichopo kibaha mkoani Pwani na kutokana na mafanikio wanaingia katika hatua ya pili ya upanuzi na uzalishaji ambapo wanatarajia katika upanuzi huu  awamu ya pili kutengeneza magari 10(trucks) kwa siku kutoka magari 4 ambayo kwa itaunganisha magari makubwa na madogo.

Meneja wa kiwandq cha kuunganisha magari cha GFA ,Ezra Mereng akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigae baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa mtengenezaji bora wa Magari kwa mwaka 2024 wa tuzo za Rais za uzalishaji bora nchini zilizofanyika jijini Dar salaam.


Pia mkakati ni kulifikia soko la ndani la nje ili kuliiingizia Taifa pesa za kigeni kwa kuuza magari katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika watumie bidhaa kutoka Tanzania jambo ambalo hapo zamani halikuzoeleka miongoni mwa magari hayo ni FAW,HONG YAN na FOLAND

Tunaipongeza serikali kuweka mazingira mazuri hasa sheria ya Local Content kuwawezesha Watanzania kufanya kazi mbalimbali na kutoa huduma migodini na miradi ya serikali hali iliyokuza vipato vya Watanzania wengi na kumudu kununua magari kutoka kiwandani kwetu alimaliza Karmali.

About Author

Bongo News

67 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *