Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema anatamani kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ipo siku kwa uwezo wa mwenyezi Mungu atavaa viatu hivyo na kuwatumikia wananchi bila kuwapo ufisadi na ukandamizwaji wa haki za wananchi
amesisitiza azma ya chama hicho kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika serikali za mitaa, endapo kitaaminiwa kuongoza.

Akizungumza Novemba 24, 2024, katika jimbo la Kasulu Mjini, mkoani Kigoma, kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, Zitto ametoa wito kwa wananchi kuwapa nafasi wagombea wa ACT Wazalendo kuongoza mitaa na vijiji vyao.

“Tunataka tuweke mazingira ambayo tunajenga vijiji vya wote kwa masilahi ya wote, mitaa ya wote kwa masilahi ya wote. Tutatumia serikali zetu za vijiji kwa taratibu za kisheria kulinda haki ya ardhi ya watu, watu walime, wavune, hakuna polisi sijui nani kuingia kuharibu mazao, hakuna watu kukamatwa hovyo, tutafanya utaratibu ambao kila mtu atafaidika. Ombi langu kwenu, tupeni mitaa ACT Wazalendo. Lengo letu sisi tunataka tuiongoze hii mitaa kwa namna ambayo tungeongoza serikali.” Ameeleza Zitto.

Zitto amesisitiza kuwa ACT Wazalendo imejipanga kuhakikisha kuwa rasilimali za wananchi zinalindwa na matumizi bora ya ardhi yanahimizwa kwa manufaa ya wote.

Aidha, ametoa hakikisho kwamba uongozi wa chama hicho utaweka kipaumbele katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa sawa na kuhakikishiwa ulinzi wa mali zao dhidi ya ukandamizaji wa kiholela.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *