Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Same na Mwanga (Samwasa) kwa kuhakikisha huduma ya maji inafika katika vitongoji vya Mahuu na Kavambughu.

Alitoa pongezi hizo baada ya kutembelea Kitongoji cha Kavambughu, ambapo alihakikisha kwamba maji yanatoka kama ilivyokuwa agizo la Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ambaye alitoa agizo hilo wiki mbili zilizopita.

Mkuu wa Wilaya alieleza furaha yake ya kuona utekelezaji wa agizo na kuwashukuru Rais Samia Suluhu Hassan , Waziri wa maji na Mkurugenzi wa Samwasa kwa juhudi zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Samwasa, Mhandisi Rashid Mwinjuma, alithibitisha kuwa zaidi ya wakazi 5000 wa vitongoji hivyo wameshaanza kupata maji safi na salama.

Alisema kuwa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95, na vituo saba vya maji vimeanza kutoa huduma.

Aidha, alieleza kuwa Samwasa inaendelea kutekeleza miradi mingine midogomidogo ya maji inayogharimu zaidi ya shilingi milioni 200 kwa lengo la kuboresha huduma za maji

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisisitiza kukamilika kwa mradi huu kumewezesha Mamlaka kufikia pia lengo la Serikali la Kufikisha huduma ya maji kwa zaidi ya 95% ya wakazi wa mjini 

About Author

Bongo News

44 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *