📌Akerwa na kusuasua kwa utendaji wa Kituo hicho
📌Awataka watendaji kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea
📌Ahoji sababu za kutelekezwa kwa maelekezo yake ya 2024
Na Mwandishi Wetu, Dar

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza kufumuliwa kwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO) kufuatia kituo hicho kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa viwango vinavyotarajiwa.
Ametoa agizo hilo leo tarehe 9 Januari, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea kituo hicho pamoja na mambo mengine kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Aprili, 2024.
Dkt. Biteko ameshangazwa na hatua ya TANESCO kuweka kando maelekezo ya mwezi Aprili 2024 yaliyolitaka Shirika hilo kuondokana na matumizi ya namba za kulipia kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (free toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ili kuwapa unafuu wananchi wanaohitaji huduma za TANESCO.

” Wewe ulishapiga simu, pesa yako ikakatwa na huduma usiipate? Wananchi wanaumia sana!” naagiza kuundwa upya kituo ili kuongeza ufanisi na tija kwa Wananchi, “kituo hiki kinategemewa na Watanzania wengi na huduma inayotolewa hapa hairidhishi kabisa,” amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Rais Samia imetoa fedha nyingi kuhudumia kituo hicho lakini utendaji wake ni mbovu kuliko huduma ya kituo.
TANESCO ilielekezwa kuachana na matumizi ya namba za kulipia Kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA ili kuwapa unafuu wa Wananchi wanapopiga kuhitaji huduma za TANESCO.

Dkt. Biteko ametoa wiki moja kwa uongozi wa TANESCO kufanya maboresho ya Kituo hicho na matokeo yake yawe wazi kwa Wananchi kutokana na huduma zake.
Akizungumzia utendaji wa Kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Abubakar Issa amesema kulikuwa na changamoto za kibajeti. Aidha amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA watakaa haraka na kuanza matumizi ya namba bila malipo ili kutoa unafuu kwa wananchi na kuleta tija kwa watumiaji.
4 Comments
Its like you read my mind You appear to know so much about this like you wrote the book in it or something I think that you can do with a few pics to drive the message home a little bit but other than that this is fantastic blog A great read Ill certainly be backHABANERO88
Hello pun appreciators!
Make your squad laugh harder than a missed free throw in overtime. basketball puns
Basketball.puns so good, you’ll need a timeout from laughing. Serve these up at your next game night.
Toda la información en el enlace – п»їhttps://basketballpuns.com/
Wishing you lots of giggles!
?Hola jugadores
Una licencia internacional puede incluir reglas contra el lavado de dinero, verificaciГіn de edad y juego responsable. No todos los casinos sin licencia son inseguros. http://casinossinlicenciaenespana.guru Lo importante es que cumplan estГЎndares.
Los pagos en casinos sin licencia son mГЎs rГЎpidos y directos. Puedes recibir tus ganancias en minutos, sin pasar por largas verificaciones.
Mas detalles en el enlace – п»їhttps://casinossinlicenciaenespana.guru/
?Que tengas excelentes ventajas!
¡Hola fanáticos de las apuestas
Plataformas de apuestas sin licencia aceptan criptomonedas y mГ©todos alternativos de pago. casinossinlicenciaenespana Esto las convierte en una opciГіn moderna y conveniente.
Los pagos en casinos sin licencia son mГЎs rГЎpidos y directos. Puedes recibir tus ganancias en minutos, sin pasar por largas verificaciones.
Consulta el enlace para más información – п»їhttps://casinossinlicenciaenespana.guru/
¡Por muchos carcajadas!