Taarifa kutoka Kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga inatueleza kuwa Watu tisa wamefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea jana usiku Septemba 22, 2023 katika mteremko mkali wa Iwambi, Wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya ikihusisha Lori na basi la abiria.
Kamanda Benjamini Kuzaga amesema katika ajali hiyo, watu tisa wamepoteza maisha na kati ya hao, wanaume ni wakiwa tano na wanawake wanne.
Amesema watu 23 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, wanaume wakiwa ni 13 na wanawake wakiwa 10, majeruhi wote katika ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya Ifisi iliyopo mji mdogo wa Mbalizi jijini Mbeya