KITAIFA

“ARUSHA YETU, KARATU YETU, UTALII WETU”

“ARUSHA YETU, KARATU YETU, UTALII WETU”

Leo Mei 24, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Arusha anapoendelea na ziara yake ya siku sita ya kutembelea wilaya zote sita za Mkoa wa Arusha ikiwa leo ni zamu ya Wilaya ya Karatu, bado ameendelea kutumia magari ya utalii kwenye ziara hiyo lengo likiwa ni kuendelea kuhamasisha na kuifungamanisha jamii ya Arusha na sekta hiyo muhimu kiuchumi na kijamii.

Kwenye Mikutano yake ya Wilaya za Mkoa wa Arusha Mhe. Mkuu wa Mkoa amehimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika kuimarisha ulinzi na usalama, kwani ndiyo kivutio kikuu cha kuvutia wageni na watalii kutembelea Mkoa wa Arusha.

Mhe. Mkuu wa Mkoa pia amekaribisha wananchi kuwekeza zaidi kwenye sekta ya utalii hasa kwenye upande wa malazi (vyumba na nyumba za kulala wageni)na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji watakaotaka kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Wakati wa kuapishwa kwake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuagiza Mhe. Mkuu wa Mkoa kuhakikisha anakuza utalii mkoani Arusha sambamba na kuongeza vyumba na vitanda kutokana na matokeo mazuri yanayoendelea kuonekana kutokana na filamu ya Rais Samia ya The Royal Tour iliyokuwa na nia ya kuitangazia dunia kuhusu vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.

About Author

Bongo News

3 Comments

    “I love how secure and seamless the Stash login process is. Convenience at its best!”

    “The layout and visuals are top-notch. It’s obvious a lot of thought went into the design.”

    “BriansClub offers an incredible network of resources—it’s truly impressive how much value you get by being part of this platform!”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *