KITAIFA

BANDARI YA KAREMA KIVUTIO ZIWA TANGANYIKA , YAKWAMISHWA NA UBOVU WA BARABARA

BANDARI YA KAREMA  KIVUTIO ZIWA TANGANYIKA , YAKWAMISHWA NA UBOVU WA BARABARA

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula

Bandari ya kimkakati, Karema iliyopo Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi ambayo imejengwa kisasa zaidi imeanza kutoa huduma za kibandari ikiwemo kupokea na kusafirisha shehena kwenda sehemu mbalimbali nchini zikiwemo nchi jirani za RDC Congo, Burundi, Zambia na kwingine.


Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula amezungumza na Waandishi wa Habari na kuweka wazi kuwa, mradi wa ujenzi wa bandari hiyo ulianza mwaka 2019 umegharimu bilioni 47.9 mpaka kukamilika, huku gati la kupaki meli likiwa na urefu wa mita 150 na kina cha mita 5.


Meneja Mabula amesema kuwa, pamoja na uzuri na ubora wa bandari hiyo bado wateja wanaoitumia ni wachache huku wengi wakishindwa kuleta shehena zao kutokana na miundombinu ya barabara inayoiunganisha bandari hiyo na maeneo zinakotoka shehena za mizigo kutokuwa rafiki.
“Tumewahi kukutana na baadhi ya wadau ambao ni wafanyabiashara, wameipenda sana bandari hii na kupongeza ujenzi wake, wanatamani kupitisha shehena zao hapa ila kila mmoja anakwambia barabara siro rafiki. Tunaamini barabara ikiwa vizuri tutapokea shehena nyingi sana.
“Eneo lote hili la bandari ya Karema lina ukubwa wa heka 60, mpaka sasa tumeshatumia heka 15, nafasi bado ipo ya kuendeleza, tutaweka pia nafasi ya vyombo vya jeshi, wenye boti ndogondogo pia watapewa nafasi, kila mtu atapata nafasi ya kufanya kazi bila wasiwasi,:” alisema Mabula.

About Author

Bongo News

42 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *