KUBORESHWA.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa (Mb) ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia Kitengo kinachoshughulikia Malalamiko yanayotolewa kwa Wizara, Taasisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha wanayafanyia kazi na kutoa mrejesho wa utatuzi wa malalamiko kwa Wananchi.
Aidha, Bashungwa amevitaka Vitengo vya Mawasiliano na Habari vya Wizara, Vyombo vya Usalama na Taasisi zote kuboresha mfumo wa Mawasiliano na habari kwa umma.
Ameeleza hayo leo tarehe 12 Disemba, 2024 wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma na kusisitiza kuwa ni haki ya Watanzania kupata taarifa sahihi kwa wakati.
“Kuna Malalamiko mengine yanakuwepo kwa sababu hamna taarifa sahihi au taarifa imechelewa, kwahiyo lazima mhakikishe mnashughulikia Malalamiko na kutoa mrejesho”, ameeleza Bashungwa.
Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara kutoa ushirikiano kwake na viongozi wengine wote ili kwa pamoja kutimiza adhima ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwahudumia Wananchi.
Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amemkaribisha Waziri Bashungwa na kumhakikishia ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa majukumu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
5 Comments
Good day I am so happy I found your weblog, I really found you by accident, while I was searching on Askjeeve for something else, Anyhow I am here now and would just like to say cheers for a remarkable post and a all round thrilling blog (I also love the theme/design), I
don’t have time to read it all at the minute but I have bookmarked it and also added in your RSS feeds, so when I have time I will be back to read much more,
Please do keep up the excellent jo.
Онлайн-сервисы открывают доступ к тысячам сериалов для любого настроения
“http://www.gaonkorea.kr/bbs/board.php?bo_table=free&wr_id=109745”
Теперь можно смотреть сериалы онлайн даже без подписки
https://magical.co.kr/bbs/board.php?bo_table=free&wr_id=348194
It’s actually a nice and useful piece of information. I’m happy
that you just shared this helpful info with us. Please keep us up to date like
this. Thanks for sharing.
I have read so many articles or reviews on the
topic of the blogger lovers but this article is genuinely a
nice article, keep it up.