Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amekagua na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na usimamizi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) km 112.3, sehemu ya Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60) kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi Kampuni ya AVIC kuwasilisha mpango kazi utakaomuwezesha kukamilisha ujenzi ifikapo mwezi Machi, 2025.
Bashungwa ametoa agizo hilo leo Oktoba 02, 2024 jijini Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ambapo amemsisitiza Mkandarasi huyo kuongeza nguvu kazi, mitambo na kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati kama ilivyopangwa kwenye mkataba.
“Naibu Katibu Mkuu, hakikisha unakaa na Mkandarasi AVIC ili tuone mpango kazi wake ambao utaonesha ujenzi wa barabara hiyo kukamilika mwezi wa tatu mwakani kama mkataba unavyotaka”, amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa amemuagiza Mkandarasi Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) anayejenga sehemu ya kwanza ya barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma kutoka Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3) kuhakikisha anakamilisha sehemu hiyo kufikia mwezi Desemba, 2024 kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika mradi huo.
Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde kusimamia kwa karibu ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma kwa kufanya ukaguzi na kutumia mikataba kuwabana Makandarasi wababaishaji na wazembe wasipewe fursa ya kupewa kazi nyingine.
Kadhalika, Bashungwa ameeleza Mikakati ya Serikali ya kupunguza msongamano na kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji katika mji wa Dodoma kwa kupanua sehemu za barabara kuu zinazoingia ndani ya jiji hilo kuwa njia nne ambazo ni barabara ya Dodoma mjini – Ikulu Chamwino, Dodoma Mjini – Msalato na Dodoma Mjini – Mkonze (SGR).
Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Msimamizi wa Mradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Herman Laswai amesema kuwa tayari Wakala umeshamuelekeza mkandarasi AVIC kutatua changamoto ya vifaa aliyonayo na tayari walishamuandikia barua ya onyo ya kutokumuongeza muda.
Kwa upande wake, Mhandisi kutoka kampuni ya Inter – Consult Eng. Deogratius Nyambo ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma sehemu ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3) kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 83.6 na umeweza kutoa fursa za ajira kwa wazawa 505.
Naye, Mhandisi kutoka Kampuni ya PACE Eng. Daniel Nila ameeleza ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma sehemu ya Ihumwa – Matumbulu – Nala (km 60) umefika asilimia 79.1.
5 Comments
protogel protogel protogel
Someone essentially assist to make significantly posts I’d state.
That is the first time I frequented your website page
and up to now? I amazed with the research you made to make this particular post extraordinary.
Excellent process!
Магазин велосипедов velosiped-internet-magazin.ru
По теме интернет магазин велосипедов Вы пришли по нужному адресу. Тут большой ассортимент велосипедов представлен в наличии и на заказ. По любому вопросу обращайтесь по телефону +7(495)215-27-98 или закажите обратный звонок. Наши специалисты ответят на все вопросы, дадут рекомендации по подбору и покупке велосипедов и аксессуаров к ним.
Веломагазин Москва velosiped-internet-magazin.ru
По запросу веломагазины мск Вы пришли по нужному адресу. Здесь большой ассортимент велосипедов есть в наличии и под заказ. По возникшим вопросам обращайтесь по номеру телефона +7(495)215-27-98 или оформите обратный звонок. Наши менеджеры ответят на любые вопросы, дадут рекомендации по подбору и приобретению велосипедов и велозапчастей к ним.
Ассортимент велосипедов velosiped-internet-magazin.ru
Если Вы планировали найти магазины велосипедов то переходите к нам. Представляем услугу зимнего хранения велосипедов в Москве по низким ценам. Для небольших квартир без подвалов или балконов очень удобно на холодное время отдать велосипед на хранение в спец место. У нас вы получите прекрасный сервис с доставкой по надобности.
Přijetí hypoteční platby může být nebezpečné pokud nemáte
rádi čekání v dlouhých řadách , vyplnění extrémní formuláře , a odmítnutí úvěru na základě vašeho úvěrového skóre
. Přijímání hypoteční platby může být problematické, pokud nemáte
rádi čekání v dlouhých řadách , podávání extrémních
formulářů , a odmítnutí úvěru na základě vašeho úvěrového skóre .
Přijímání hypoteční platby může být problematické ,
pokud nemáte rádi čekání v dlouhých řadách , vyplnění
extrémních formulářů a odmítnutí úvěrových rozhodnutí založených na úvěrových skóre
. Nyní můžete svou hypotéku zaplatit rychle a efektivně v České
republice. https://groups.google.com/g/sheasjkdcdjksaksda/c/sFLL7Q2TM40