Na Rahel Chizoza, Mwanza

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Boti ya doria ambayo itatumika kupambana na magendo katika ZiwaVictoria na kukomesha vitendo vya ukwepaji kodi ambavyo vimekuwa vikifanywa na watu wasioitakia Tanzania.

Uzinduzi wa Boti hiyo ya Doria umefanywa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe Hamad Chande mkoani Mwanza na kueleza kuwa ujio wa Boti hiyo ya kisasa utakomesha magendo yanayofanyika katika Ziwa Victoria.

Mhe. Chande amesema kila Mtanzaia kwa nafasi yake anapaswa kupambana na magendo maana yanaliumiza Taifa Zima na siyo TRA peke yao kama wengi wanavyodhani maana kodi wanayokwepa wafanya magendo, ingeweza kufanya shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.

Amesema uwepo wa Meli hiyo na nyingine zilizopo katika maziwa mengine na baharini utasaidia kuokoa mapato yaliyokuwa yakipotea kutokana na uingizwaji wa bidhaa bila kufuata utaratibu.

About Author

Bongo News

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *