KITAIFA

BUMBULI WACHEKELEA UTEKELEZWAJI WA MIRADI, WAMPONGEZA RAIS SAMIA

BUMBULI WACHEKELEA UTEKELEZWAJI WA MIRADI, WAMPONGEZA RAIS SAMIA

Raisa Said,Bumbuli

Madiwani Wa Halmashauri ya Bumbuli Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kuwapelekea Miradi ya Maendeleo katika kata zao wanazo ziongoza.

Pia Madiwani hao wametoa shukrani kwa Mbunge wao January Makamba kwa kuendelea kupigania Maendeleo na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi

Shukrani hizo wamezitoa wakati Wa kikao Cha Tathimini kilichofanywa na ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo ambapo walisema katika Kipindi Cha miaka mitatu ya serikalj ya awamu ya sita Kuna Miradi mingi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la bumbuli.

” Licha ya Kumshukuru Rais kwa kutupatia fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri yetu lakini pia tunashukuru Mbunge wetu January Makamba kwa kuhakikisha tunapata Miradi mingi ya Maendeleo katika Halmashauri yetu ya Bumbuli” wamesema.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Wa Mbunge wa Jimbo Hilo Hoza Mandia alisema kuwa wao kama ofisi ya Mbunge wamekuwa na utaratibu Wa kila Mwaka kufanya kikao cha Tathimini kuangalia walipo na wanapokwenda nakuongeza kuwa kwakuwa wanaelekea kwenda kwenye vikao vya Bajeti ktk halmashauri yao waone ni maeneo yapi yawekewe kipaumbele ili kuleta uwiano wa kata zao zisipishane kimaendeo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto Ally Daffa amewapongeza madiwani hao kwa kuona umuhimu Wa kufanya Tathimini huku akiahidi utaratibu huo ataupeleka maeno mengine ndani ya Wilaya yake.

Daffa alisisitiza kuwa licha ya kupongeza kupata Miradi hiyo ya maendeleo lakini aliwataka wananchi walioko nje ya Bumbuli kuhakikisha wanafika kujionea namna Miradi inayotekelezwa badala kuzungumza bila kuona.

Halmashauri ya Bumbuli katika Mwaka Wa fedha Wa 2022 / 23 wamepokea kiasi cha fedha za Miradi ya Maendeleo katika sekta ya elimu ,afya na utawala kiasi cha sh.5,023,835,638 na Kwa Mwaka 2023/2024 hadi kufikia January wamepokea kiasi Cha 2,238,815
,879

About Author

Bongo News

33 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *