Halmashauri ya Bumbuli, Mkoani Tanga, imefanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kupata asilimia 105.7.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Baraka Zikatimu, alifafanua kuwa lengo lilikuwa kuandikisha watu 88,395, lakini walioandikishwa ni 93,392.
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alisema kuwa kambi yake ya hamasa, kwa ushirikiano na viongozi wa chama na serikali, imechangia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo hilo.
Alisisitiza kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, Jimbo la Bumbuli haitapoteza kiti chochote
Makamba aliwataka wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi ifikapo siku ya upigaji kura tarehe 27 Novemba mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa waTanga Balozi Batilda Buriani alisema kuwa mkoa wa Tanga umeshika nafasi ya pili katika uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa kupata asilimia 110 .82 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkoa wa Pwani uliopata asilimia 112.61 pwani.
Hata hivyo Balozi Batilda alitumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa mkoa watanga kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
2 Comments
Malatya uydu montajı Uyducu Malatya, sorunumuzu hızlıca çözdü, gerçekten işlerini biliyorlar. https://www.nitrnd.com/blogs/193470/Malatya-%C3%87anak-Anten-ve-Uydu-Onar%C4%B1m%C4%B1
I am glad to be a visitor of this perfect web site! , appreciate it for this rare information! .