KITAIFA

DC MPOGOLO: WANASIASA HAWANA NIA YA KUMFIKISHA RAIS SAMIA KWENYE MALENGO YAKE

DC MPOGOLO: WANASIASA HAWANA NIA YA KUMFIKISHA RAIS SAMIA KWENYE MALENGO YAKE

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amefanya mahojiano na waandishi wa habari leo tarehe 22 Juni 2023 katika ofisi zake jijini Dar es Salaam. Katika mahojiano hayo, amezungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na majukumu yake ya kazi, huku akitoa ufafanuzi kuhusu uwekezaji katika bandari.

Mpogolo amesisitiza kuwa Rais Samia ana malengo na lengo lake liko katika ilani ya uchaguzi. Amewakumbusha wananchi kuwa Rais Samia aliwaahidi miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na serikali, ikiwa ni pamoja na eneo la bandari, mradi wa reli, upatikanaji wa umeme, ajira, na miradi mingine.

“Mkataba ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameuweka Kwa wananchi kwa miaka mitano unalenga miundombinu ya nchi Sasa hao wanasiasa ambao wanaopinga hawana malengo wanachokitaka ni kumfanya Rais Samia Suluhu Hassan asifikie Katika malengo kwasababu wanajua akifika Katika malengo watanzania watampa mitano tena na kumfanya ni kumzuia Katika malengo ambayo anataka kuyafikia”. Alisema mpogolo

Mpogolo ameeleza kuwa mkataba ambao Rais Samia ameuweka kwa wananchi kwa miaka mitano unalenga kuimarisha miundombinu ya nchi. Amewalaumu wanasiasa ambao wanapinga hatua hizi, akisema kuwa hawana malengo ya maendeleo na wanajaribu kumzuia Rais Samia kutimiza malengo yake. Anadai kuwa wanajua ikiwa Rais Samia atafikia malengo yake, wananchi watampa kipindi kingine cha uongozi, na hivyo, wanajaribu kumzuia Rais asifikie malengo hayo.

About Author

Bongo News

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *