KITAIFA

DKT. MSONDE AELEKEZA NGUVU KAZI IONGEZWE UTEKELEZAJI MIRADI YA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIKONGE NA TABORA MANISPAA

DKT. MSONDE AELEKEZA NGUVU KAZI IONGEZWE UTEKELEZAJI MIRADI YA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIKONGE NA TABORA MANISPAA

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akisisitiza jambo wakati akikagua ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Milambo iliyopo Manispaa ya Tabora.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Dkt. Charles Msonde amewaelekeza viongozi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge na Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanawasimamia
mafundi kuongeza nguvu kazi itakayowezesha kukamilisha ujenzi wa
miradi ya miundombinu katika shule za msingi na sekondari ili wanafunzi
wanufaike na miundombinu hiyo.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akihimiza ukamilishaji wa mradi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Msingi Kiniga, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.


Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo kwa nyakati tofauti akiwa wilayani
Sikonge na Manispaa ya Tabora, mara baada ya kuhitimisha ziara ya
kukagua utekelezaji wa mradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule za
msingi na sekondari katika halmashauri hizo.
Dkt. Msonde amewata viongozi hao kuhakikisha ndani ya siku mbili katika
maeneo yote ambayo ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na
sekondari unaendelea, kunakuwa na mafundi wa kutosha ili kukamilisha
miradi hiyo kwa wakati.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akiwasilisi kukagua moja ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya elimu  katika Manispaa ya Tabora.

“Nimetembelea ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari, hususani
shule ya sekondari Kamagi na nimejionea ujenzi katika shule hiyo upo
hatua ya msingi ambayo ina kwamisha lengo la Serikali,” Dkt. Msonde
amesisitiza.
Dkt. Msonde ameongeza kuwa, changamoto ya upungufu wa mafundi
kama zilivyo nyinginezo inapaswa kutatuliwa na viongozi hao wa Sikonge
na Manispaa ya Tabora kwani ni wajibu wao viongozi kuitatua o ili miradi
ikamilike kwa wakati.
Dkt. Msonde amehimiza kuwa, ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu
inapaswa kuwa ya kudumu ili itumiwe na vizazi vingi, hivyo Serikali
haitarajii miundombinu hiyo ikikamiliza ichakae ndani ya muda mfupi na
kuilazimu tena kutafuta fedha nyingine za kujenga miundombinu mipya.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sikonge, Bw. Selemani Pandawe amesema, yeye pamoja na watumishi
anaowaongoza watajipanga kikamilifu kutekeleza maelekezo ya Dkt. Msonde ya kusimamia vema ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu ili
kuboresha utoaji wa elimu ya msingi na sekondari katika halmashauri yake.

Mafundi wakiendelea na ujenzi miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Kazima iliyopo Halmashuri ya Manispaa ya Tabora.


Dkt. Msonde amekagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya elimu
kwenye shule ya Sekondari Kamagi, Shule ya Sekondari Kiwere, Shule ya
Msingi Matale na Kiniga zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ikiwa
ni pamoja na Shule ya Msingi Mabatini, Shule ya Msingi Magereza na
Shule za Sekondari za Milambo na Mabatini zilizopo Manispaa ya Tabora.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *