KITAIFA

DKT. MWIGULU ASEMA MKUTANO WA AFRIKA HUMAN CAPITAL UMEKUJA WAKATI MUAFAKA

DKT. MWIGULU ASEMA MKUTANO WA AFRIKA HUMAN CAPITAL UMEKUJA WAKATI MUAFAKA

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo ametembelea katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam utakapofanyika mkutano mkubwa, Africa Human Capital, utakaowakutanisha wakuu wa nchi za Afrika kuanzia Julai 25-26, 2023 kuangalia maandalizi na kusema kuwa umekuja wakati muafaka.

Akizungumza baada ya kutembelea katika ukumbi huo, Dkt. Mwigulu kwanza alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa unaobeba masuala ya rasilimali watu ambao unalenga katika kukuza uchumi imara unaozingatia ujifunzaji mzuri wa vijana na kuongeza tija kwenye uzalishaji kupitia nguvu kazi ya vijana.

“Mkutano huu umekuja wakati muafaka  kipindi ambacho Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nguvu kubwa katika masuala ya kukuza rasilimali watu, utaona Mhe. Rais ameweka mazingira bora ya elimu bila malipo kuanzia madarasa ya chini mpaka kidato cha sita, katika kipindi hicho hicho ameweka elimu bila malipo mpaka kwenye vyuo vya ufundi, ameweka utaratibu wa wanafunzi kupata mikopo kwa kuanza kwenye ngazi ya vyuo vya kati, lakini pia ameongeza kwa takribani mara mbili mikopo ya elimu ya juu ikiwa inamaanisha wigo mpana wa wanafunzi wanaokwenda kupata elimu ngazi zote nilizozitaja,” amesema.

Aidha Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa na lengo kubwa la kuwekeza katika uchumi wa kidigital na kuhakikisha unapewa msukumu mkubwa, ndio maana alivyoapa tu aliweko ‘focus’ ya kujenga chuo cha TEHAMA hiyo yote ikiwa ni kukuza masuala ya kidigital katika nchi yetu, ukiangalia haya yote wenzetu wa Benki ya Dunia waliona kwamba, mada hiyo ambayo wanaandaa na umuhimu mkubwa ambao Serikali inaweka katika masuala ya Human Capital, ingefaa Tanzania kuwa mwenyeji, ukiangalia yote ambayo Mhe. Rais na Serikali yake wanafanya unaona kwamba ni sifa za kutosha Tanzania kuwa mwenyeji wa jambo hili kubwa.

“Maandalizi yote yamekamilika na kama unavyoona kuanzia hapa kwenye mkutano, masuala ya mapokezi, masuala ya namna ya ‘kuwahost’ wageni wetu pamoja na ukumbi wa mikutano pamoja kumbi za mikutano midogo ambayo itafanyika, maandalizi yote yako tayari kwa ajili ya kupokea ugeni. Niwakaribishe wote, Watanzania pamoja na wageni wanaokuja, wakishamaliza masuala ya mkutano ambayo yalikuwa hapa Dar es Salaam wapate fulsa pia kufanya shughuli nyingine za kiutalii, tuna vivutio vya asili, Makumbusho, tuna Zanzibar, tuna Kilimajaro, Ngorongoro, Serengeti, pia wanaweza kwenda kushuhudia ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere,” amesema Mwigulu.   

        

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *