KITAIFA

DKT. TULIA AWATAKA WANANCHI KUWAKATAA WAPINGA MAENDELEO

DKT. TULIA AWATAKA WANANCHI KUWAKATAA WAPINGA MAENDELEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka
Wananchi kote nchini kunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali
yao kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na kuwapuuza wale wote
wanaowashawishi kuyapinga.
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 5 Agosti, 2023 wakati akifanya
mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Mwakibete Jijini
humo kwa lengo la kuwaeleza mambo aliyoyafanya katika kipindi
chake cha Uongozi katika Jiji hilo na yale yaliyofanywa na Serikali ya
awamu ya sita.


Akitolea mfano wa baadhi ya maendeleo yaliyofanywa katika Jiji hilo
ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango
cha lami na zaidi kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa barabara kuu ya
njia nne kutoka Igawa hadi Tunduma KM 218 ambapo tayari Serikali
imeshatenga Shilingi bilioni 218 na mchakato wa ujenzi umeanza.
Katika sekta ya maji, Dkt. Tulia amewaeleza Wananchi kwamba
Serikali imeshatoa Shilingi Bilioni 119 kwa ajili ya kusambaza maji
kupitia mradi wa mto Kiwira ambao utasaidia kumaliza changamoto
hiyo kwa Jiji la Mbeya na Mkoa kwa ujumla.
Kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Dkt. Tulia amewatoa
hofu Wananchi kuhusu wanaopotosha kwa makusudi wakidai
kwamba imeuzwa na badala yake amewaeeleza kuwa kinachofanyika
ni ushirikiano wa kibiashara ambao utawezesha nchi kuongeza
mapato yake na kusaidia kuharakisha maendeleo yao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,
amewataka Wananchi wa Jimbo la Mbeya kujivunia na kumuombea
Dkt. Tulia ili aendelee kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa

kwa miaka mingi kutokana na kuibadilisha siasa za Jiji hilo zilizokuwa
za kiharakati zaidi na sasa amezifanya kuwa za kimaendeleo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *