Wakati maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yakiwa yanafunguliwa leo Julai 03,2024, mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan walitembelea mabanda mbali mbali kabla ya kuyafungua rasmi.
Miongoni mwa makampuni yaliotembelewa na Maraisi hao ni pamoja na banda la kampuni ya GF Group ambao ni wauzaji wa magari na mitambo ya ujenzi na migodini.
Akizungumza wakati Marais hao wakiwa akatika banda lao Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd , Imrani Karmali amesema wao baada ya ziara ya Rais nchini Korea kushawishi wawekezaji kuwekeza nchin walianza harakati zao zwa kuwashawi.
Amesema kiwanda chao cha kuunganisha magari cha GF Assembling wamezungumza na wakorea na wako tayari kuja kuunganisha magari aina ya Hyundai nchini lakini wamewataka GF kuwa na oda zaidi ya magari 300 kwa kuanzia ndipo wakorea hao watoe idhini ya kufunga kiwanda cha kuunganisha magari hayo
“sisi kama GFA tupo tayari lakini tunaiomba Serikali kupitia Wizara na tasisi zake kutuunga mkono katika hili kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa na uhakika na matunda ya ziara yako nchini korea yatakuwa yameonekana kwa Hyundani kutengenezwa nchini Tanzania”