Dar es Salaam. Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya uendeshaji wa michezo ya bahati nasibu za taifa barani Afrika, ITHUBA Africa pamoja na kampuni ya Kitanzania, SF Group.

Hatua hiyo inatokana na kampuni hizo mbili kushinda tenda ya kuendesha michezo ya bahati na simu na hivyo kukabidhiwa rasmi leseni ya uendeshaji wa mchezo wa Bahati Nasibu ya Taifa kwenye hafla fupi iliyofanyika juzi katika ofisi za Bodi ya Michezo ya Kubahatisha jiijni Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa ITHUBA Erick Mabuza (kushoto) akipokea leseni uendeshaji wa michezo ya bahati nasibu ya Taifa kutoka kwa 
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia wakati wa makabidhiano hayo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa ITHUBA, Charmaine Mabuza alisema wanayofurahi kuungana na SF Group.

Mabuza alisema kupitia uwekezaji wa dola za kimarekani 20milioni ( zaidi ya Sh 52bilioni) uliofanywa na ITHUBA na SF Group, wamedhamiria kuleta mapinduzi katika soko la michezo ya bahati nasibu kupitia ubunifu katika usanifu wa jukwaa la michezo hiyo.

Alisema ITHUBA Afrika na SF Group, zinatarajia kuendesha michezo wa bahati nasibu, baada ya kukamilisha mchakato huo ambapo watasajili wafanyabiashara mbalimbali ambao watauza tiketi za bahati nasibu kwa reja reja na jumla na kutakuwa na viwango na aina ya mchezo unao shindaniwa.

Makabidhiano hayo ni hatua muhimu katika kufikia dhamira ya ITHUBA ya kuchagiza maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika.

Hata hivyo, makabidhiano hayo ya leseni yalitanguliwa na hafla ya utiaji saini iliyofanyika mwezi uliopita na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa ITHUBA na SF Group wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SF Group, Kelvin Koka.

Wengine waliohudhuria hafla ya utiaji saini ni pamoja na wajumbe wa Bodi, Mkurugenzi Mkuu, pamoja na Menejimenti ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Modest Mero.

“Tunayo furaha kubwa kuungana na SF Group na kutuwezesha kuunganisha teknolojia na ujuzi wetu pamoja na uzoefu wao wa soko la Tanzania” alisema na kuon

“Wapenzi wa mchezo wa bahati nasibu hapa Tanzania wataweza kushiriki katika michezo ya kipekee kupitia jukwaa lililoundwa maalumu kwa ajili ya soko la Tanzania. Washiriki watapata fursa ya kucheza michezo mipya ya kusisimua na kupata ofa mbalimbali ambazo pia zitachangia katika kuleta mabadiliko kwenye uchumi wa jamii.”

ITHUBA na SF Group wanajipanga kuwakaribisha wafanyabiashara kujisajili kama wauzaji wa bidhaa za ITHUBA hapa nchini.

Wafanyabiashara watanufaika na malipo ya kamisheni na pia kuvutia wateja zaidi katika maduka yao kutokana na mauzo ya tiketi za bahati nasibu.

Kwa upande wake, Balozi Mero alikaribisha ITHUBA pamoja na SF Group kusukuma gurudumu la michezo hiyo nchini; “Tunayo furaha kuikaribisha ITHUBA iliyoingia ubia na kampuni ya Kitanzania, SF Group kuendesha michezo ya bahati nasibu ya taifa”. Alisema.

Mero alisema ubia wao ni fursa nzuri ya kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kupitia mapato yatakayotokana na michezo ya bahati nasibu ya taifa.

“Tuna shauku kubwa kufanya kazi kwa ukaribu na ITHUBA ili kuleta mabadiliko chanya na kuboresha maisha ya Watanzania.” Alisema Mero.

Kwa ujio wa ITHUBA nchini Tanzania, mchezo wa Bahati Nasibu ya Taifa utakuwa kichocheo katika kubadilisha maisha na kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa Watanzania.

About Author

Bongo News

2 Comments

    ktqqfn

    Its superb as your other blog posts : D, thankyou for posting. “For peace of mind, we need to resign as general manager of the universe.” by Larry Eisenberg.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *