Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Jerry Slaa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC leo Julai 12, 2023 ameamua kufunguka kuhusu sakata linaloendelea hivi sasa kuhusiana na uboreshaji na uwekezaji kwenye Bandari ya Da es Salaam.
Akiongea na Waandishi wa Habari katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam Slaa amesema kuwa kuna watu wachache walioamua kupotosha umma kuhusiana na suala la uwekezaji wa bandari kwa sababu wanazozijua wao, huku Watazania wengi wenye nia njema ambao wakiwasikia wanayoyasema inawatengenezea taharuki.
“Nimeona upotoshaji umekuwa mkubwa na Watanzania wanahitaji majibu. Kuna watu wanatumika kwa jitihada kubwa za kumuondoa Rais wetu kwenye reli ambaye anafanya jitihada kubwa za kujenga uchumi wa taifa letu. Ukiwasikiliza wengi mtu anaongea kwa dk 15 lakini hakuna sehemu yoyote anafika kuzungumzia yale makubaliano yenyewe ambayo ndiyo yalioingiwa baina ya Serikali yetu na Dubai, wanafanya hivyo makusudi ili kutengeneza sintofahamu na taharuki kwa wanachi.
“Wanahama kwenye makubaliano yenyewe wanaenda kwenye hoja za kimtaani na kutengeneza hofu. Nchi yetu imewahi kufanya ubinafsishaji maeneo mengi. TBL imebinafsishwa leo inaajiri watanzania wengi, inanunua Shairi, inalipa kodi kubwa. NMB ilibinafsishwa mwaka 2004 kulikuwa na kelele nyingi, benki ambayo ilikwa inatoa gawio la bilioni nne leo wanatoa gawio la bilioni 45.5, imeajiriwa watanza zaidi ya 2800 nchi nzima , imelipa kodi ya bili 45.3, imeajiri Watanzania zaidi ya 2800 na CO NMB ni Mtanzania, ina matawi 280, inatusaidia wote kwenye shughuli za kibenki, mifanio ipo mingi,” amesema Slaa.
Vilevile akatoa mfano wa Uwaja wa ndege wa Julius Nyerere pale Dar es Salaam ambao unamilikwa na Serikali kupitia mamlaka ya Viwanja vya Ndege ‘Tanzania Airport Authority’ lakini ukienda kuangalia uendeshaji wake unafanywa na sekta binafsi kupitia makampuni kama Swissport
na NAS
“Mimi kama mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi ninayo ahadi kwamba nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Kama nina elimu, ninao wajibu wa kutoa mtazamo ambao ni sahihi kwa ajili ya ‘consumption’ ya Watanzania pale ninapoona jambo linapotoshwa. Pia mimi kama mwenyekiti wa kamati na jambo hili lilipita kwenye kamati na katiba yetu inatoa nguvu kwa Bunge kuishauri na kuisimamia Serikali,” alisema.
1 Comment
sex ドールdon’t forget to let your partner know that you have accepted their right swipe for life.11.