KITAIFA

KAMBI MAALUMU YA UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO MKOANI DAR ES SALAAM

KAMBI MAALUMU YA UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO MKOANI DAR ES SALAAM

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam watafanya kambi maalumu ya  upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo  kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Upimaji huu ufanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 02/09/2023 hadi tarehe 03/09/2023 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili  jioni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.

Aidha katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa. Huduma hii itakuwa  ya kuchangia gharama za matibabu.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754578190 Dkt. Tulizo Shemu, 0684345921 Flaviana Masegesa, 0783922571 Irene Charles na 0674179036 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *