Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza wakuu wa kampuni za China zinazojenga barabara za Dar es Salaam kufika nchini kwa mazungumzo na serikali ili kuongeza kasi ya kukamilisha miradi hiyo.

Ulega ametoa maagizo hayo leo Machi 5, 2025, wakati akikagua miradi ya ujenzi wa barabara za mwendokasi jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, amebaini changamoto mbalimbali zinazosababisha kusuasua kwa miradi hiyo licha ya kuwa fedha za ujenzi tayari zimeshatolewa.

Miongoni mwa matatizo makubwa aliyoyaona ni kucheleweshwa kwa fedha hizo kuletwa Tanzania kwa sababu akaunti za kampuni husika ziko nchini China. Hali hiyo imekuwa ikikwamisha utekelezaji wa miradi kwa wakati.

“Barabara hizi tunazijenga kwa mikopo, na muda wa kulipa mikopo hiyo ukifika, italazimu tulipe hata kama miradi haijakamilika. Hii ni mzigo kwa wananchi mara mbili. Naomba wakandarasi wahakikishe miradi hii inakamilika kwa wakati kama tulivyokubaliana,” alisema Ulega.

Amesema atashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ili kuhakikisha wakuu wa kampuni hizo wanakuja nchini na kueleza kwa nini miradi inachelewa.

“China ni marafiki zetu wa kufa na kuzikana, na ndiyo maana ni muhimu kuambiana ukweli na kutendeana haki,” aliongeza.

Miradi ya ujenzi wa barabara za mwendokasi jijini Dar es Salaam inaendelea kusuasua licha ya fedha za ujenzi kutolewa

. Barabara zinazohusika ni Bagamoyo (Maktaba – Mwenge), Mwenge – Tegeta, na Ubungo – Kimara.

Katika ukaguzi wa barabara ya Ubungo – Kimara, Waziri Ulega amebaini kuwa kampuni ya Sichuan kutoka China haijaweka mtambo wa kutengeneza lami kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.

Pia, amegundua kuwa baadhi ya maeneo ya ujenzi hayana wasimamizi rasmi wa ujenzi kinyume na makubaliano ya mkataba.

“Fedha zinazoelekezwa kwenye miradi hii zinaweza kutumika katika maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa. Rais Samia Suluhu Hassan ametenga fedha hizi kwa sababu anajua umuhimu wa miundombinu bora katika kukuza uchumi wa taifa,” alisema Ulega.

Ameeleza kuwa kuna mradi uliopaswa kuwa umekamilika kwa zaidi ya asilimia 60, lakini hadi sasa uko asilimia 23 tu.

“Hili si jambo zuri kwa taifa linalojijenga kiuchumi. Wananchi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla wanahitaji barabara hizi zikamilike kwa wakati,” alisisitiza.

Katika ziara hiyo, Waziri Ulega aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Ujenzi, Wakala ha Barabara (TANROADS), na viongozi wengine wa serikali

About Author

Bongo News

5 Comments

    It’s nearly impossible to find educated people on this topic,
    however, you seem like you know what you’re talking about!
    Thanks

    If you desire to take a great deal from this piece of writing then you have to apply these techniques to your won website.

    It’s wonderful that you are getting ideas from this post as well as from our argument made at this time.

    Привет, если вы разыскиваете игровые автоматы, какие действительно дарят крупные выигрыши, ты попали по адресу! Наша команда сделали для вас топ-5 слотов, какие за последний месяц сотворили наших участников более радостными. Это все не есть просто слова – данные действительности, основанные в реальной исчислении выплат.

    Применяйте льготы и фриспины ради тестирования новых автоматов.

    Испытайте данные игровые автоматы на интернет-сайте Flagman — а, возможно, следующий крупный приз будет вашим!

    Привет, если ты ищете игровые автоматы, которые действительно приносят крупные выигрыши, вы очутились как раз адресу! Мы сделали для вас лучшие 5 игровых автоматов, которые в последний месяц сотворили наших игроков более радостными. Это не есть просто слова – данные факты, базирующиеся на реальной исчислении вознаграждений.

    Применяйте льготы и бесплатные вращения ради испытания свежих автоматов.

    Попробуйте данные игровые автоматы на сайте Casino Flagman — и, вероятно, следующий большой выигрыш будет твоим!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *