Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro alipokuwa akifungua mafunzo maalum juu elimu ya ukopaji yaliyoandaliwa na Chama hicho kwa udhamini wa Benki ya Uchumi na Biashara (UCB) yenye makao yake makuu mkoani Kilimanjaro pamoja na Taasisi iitwayo We Effect yenye makao yake jijini Nairobi Kenya.
Alisema kuwa Chama hicho chenye wanachama zaidi ya 1,000, wengi wao wakiwa Walimu na watumishi wa umma imeleta tofauti kwa kuwawezesha watumishi hao kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo yao.
Alisisitiza juu umuhimu wa elimu kabla ya kukopa na kusema inawafundisha wanachama kukopa na kutumia fedha kwa mujibu wa mipango na malengo na kurezirejesha kwa uaminifu ili watu wengine waendelee kufaidika na huduma ya mikopo.
Aliipongeza uongozi wa Chama hicho chini ya Dk Godwin Maimu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho kwa kufikiria kuanzisha mafunzo ya aina hiyo ambayo ni muhimu kwa kuweka nidhamu ya matumizi na kuhakikisha kuwa mikopo hiyo inawapa faida wakopaji.
Akizungumzia katika semina hiyo, Dk Maimu alishukuru serikali inayoongozwa Rais Dark Samia Suluhu Hassan kwa kuweka miongozo ambayo inatoa mwanya wa Taasisi za fedha kutoa mikopo ya riba rafiki kwa Taasisi za wananchi kama SACCOS.
Dk Maimu alisisitiza, hata hivyo juu ya umuhimu wa mafunzo kuhusu kukopa kwa busara.
Alisema mpango huo wa mafunzo ni mpango endelevu ambapo kila katika robo ya mwaka watakuwa wakitoa mafunzo hayo kabla ya kukopa.
Aliishukuru Benki ya UCB kwa kukubali kutoa mikopo ambayo itaimarisha Chama hicho kutokana na changamoto ambayo chama ilipata na iliyofanya kiyumbe.
Alisema kuwa leo wamekabidhiwa hundi ya Sh milioni 200 ambazo zimetolewa na UCB kwa ajili ya mikopo kwa watumishi wa serikali ambao ni wanachama wa Chama hicho. Pia wajasiriamali wanachama watapokea mikopo yenye jumla ya sh mlioni 50 kutoka vyanzo vya ndani vya chama hicho ambacho kina leseni faraja B inayokiruhusu kufanya kazi mahali popote Tanzania.
Dk Maimu alisema kuwa mwezi April chama hicho kitapokea Sh milioni 300 kwa ajili ya mikopo kwa wajasiriamali ambao ni wanachama.
Alidokeza kuwa mwezi Juni pia watapokea fedha nyingine kwa ajili kukopesha wanachama ambapo kutakuwepo na mafunzo mengine ya aina hiyo.
Naye Meneja wa Uchumi na Biashara wa Benki hiyo, Israel Lyatuu alisema Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 itaendelea kufanya kazi na vyama vya ushirika zikiwemo SACCOS ili kuwasaidia wananchi kujikwamua kutoka katika umaskini.
Chama cha Kuweka na Kukopa Cha Lushoto Teachers Saccos Ltd kimetoa mkopo wa Shilingi million 200 kwa wanachama wake Lengo kuwainua kiuchumi.
Akizungumza mara baada ya kikabidhi Hundi, Mwenyekiti wa Bodi ya chama hicho Dk Godwin Maimu alishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuweka miongozo ambayo inatoa mwanya wa Taasisi za fedha kutoa mikopo ya riba rafiki kwa Taasisi za wananchi kama SACCOS.
Mbali na kikabidhi Hundi pia walitoa mafunzo maalum juu elimu ya ukopaji yaliyoandaliwa na Chama hicho kwa udhamini wa Benki ya Uchumi na Biashara (UCB) yenye makao yake makuu mkoani Kilimanjaro pamoja na Taasisi iitwayo We Effect yenye makao yake jijini Nairobi Kenya.
Alisema kuwa Chama hicho chenye wanachama zaidi ya 1,000, wengi wao wakiwa Walimu na watumishi wa umma imeleta tofauti kwa kuwawezesha watumishi hao kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo yao.