Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) imehitimisha mafunzo ya siku tatu katika
chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) ambapo kimetoa elimu ya ukatili na
sheria zinazosimamia vitendo vya ukatili.
Akiongea mara baada ya mafunzo hayo mratibu wa dawati la jinsia Taasisi ya
maendeleo ya jamii Tengeru Prisca Kadege ametoa ushauri kuwa madawati hayo yawe
nyenzo ya utoaji wa elimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ni vyema wahusika
katika madawati hayo kuwa wabunifu ili kufikia makundi yote ndani ya jamii katika
kukabiliana na ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake mwakilishi wa dawati la jinsia chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es
salaam mrakibu msadizi wa Polisi ASP Lucy Kiluka amebainisha kuwa mafunzo hayo
yamewaongezea maarifa na chachu katika mabadiliko ya utendaji kazi wa madawati ya
jinsia.
Nae Mhadhiri msadizi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Elinami Nassari
amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea umahiri wa kutambua maswala
ya jinsia kwa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Wakili Renatus Mgongo kutoka Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru, kitengo cha
sheria amewaomba wananchi kushirikiana na vyombo vinavyosimamia ukatili wa kijinsia
kutoa taarifa ya matukio hayo kwa Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Gift Msowoya
amewashukuru wawezeshaji hao kutoka taasisi hiyo kwa namna ambavyo
wamebadilishana maarifa katika kupambana na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.
Mwisho mkuu wa idara ya jinsia na Maendeleo kutoka Tasisi ya maendeleo ya jamii
Tengeru amesema maofisa hao wanafunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es
salaam wamepata fulsa pia ya kupitia sheria zinazosimamia ukatili wa kijinsia