Dkt. Rehema Marando ambaye ni Daktari Bingwa mbobezi wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Kitengo cha watoto wachanga amesema ndani ya kipindi cha miaka mitatu (3) serikali imefanya maboresho makubwa kwenye kitengo hicho kwa kufunga mitambo ya kisasa inayosaidia kunusuru maisha ya watoto wachanga wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuzaliwa kabla ya wakati, matatizo ya moyo, figo nk.
Amesema malengo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinapungua kwa takribani vifo 12 kwa vizazi hai 10000 hadi kufikia mwaka 2030, ambapo Tanzania imefanikisha kupunguza vifo hivyo kwa takribani vifo 24 kwa vizazi hai 1000
Dkt. Rehema amesema hapo awali kabla ya kufungwa kwa mitambo hiyo na kuletwa Madaktari Bingwa wa watoto waliobobea kwenye maeneo tofaut zzzi, watoto waliokuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali baada ya kuzaliwa ililazimika kupelekewa Hospitali ya Taifa (Muhimbili) jambo ambalo wakati mwingine lilikuwa linahatarisha maisha ya watoto hao kutokana na kuchelewa kupata huduma
1 Comment
hello!,I like your writing very much! share we communicate more about your article on AOL? I require an expert on this area to solve my problem. May be that’s you! Looking forward to see you.