KITAIFA

MAJALIWA ATEMA CHECHE,  MIMBA ZA WATOTO WA SHULE HAZIKUBALIKI. TUTAKULA NAO SAHANI MOJA

MAJALIWA ATEMA CHECHE,  MIMBA ZA WATOTO WA SHULE HAZIKUBALIKI. TUTAKULA NAO SAHANI MOJA

Ahoji ni kwa nini kesi mbili tu ziko mahakamani, awataka RC, Ma-DC wachukue hatua kwa wahusika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael na Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo wahakikishe wanawasaka watu wote wanaotuhumiwa kuwapa mimba watoto wa kike.

“Tangu Januari hadi sasa, mkoa huu una kesi 59 za wasichana walioacha shule kwa sababu ya ujauzito lakini ni kesi mbili tu zimeeenda mahakamani. Hizo 57 ziko wapi au zimeishia wapi? Ni nani anazuia kesi hizi zisiende? Jeshi la Polisi, ni kwa nini hatuwafikishi watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria?, amehoji.

“RC na Ma-DC wote kaeni na Kamati zenu za Ulinzi mbainishe wahusike na mhakikishe hatua kali zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika,” amesema Waziri Mkuu leo (Alhamisi, Novemba 23, 2023) wakati akitoa agizo hilo mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ileje.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani humo kwa ziara ya siku tatu, amesema taarifa za mkoa huo siyo kwani kesi hizo 59 ni kwa shule za sekondari na hazijumuishi shule za msingi.

Amewakemea vijana wanaopenda kutembea na watoto wa shule waache tabia hiyo mara moja kwani wanakatisha maisha ya baadaye ya watoto hao. “Sheria iko wazi katika kosa hili. Adhabu yake ni miaka 30, kijana kabla hujamfuata binti jiulize una miaka mingapi, sababu tukikufunga utarudi ukiwa mzee,” amesema.

Akisisitiza haja ya kuwalinda mabinti, Waziri Mkuu amesema: “Hawa ni watoto wetu, tunapaswa tuwalee ili wakue na kuja kushika majukumu ya nchi. Rais Samia amewekeza kwao kwa kutoa elimu bila ada. Tunapaswa tuhakikishe wanatimiza ndoto zao, kwa hiyo tuwalee ili waweze kuhitimu,” amesisitiza.

Amewaomba masheikh na wachungaji wakemee tabia hiyo kupitia mahubiri ya kwenye ibada.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewapongeza wana-Ileje kwa kujenga maabara ya kompyuta kwenye shule hiyo yenye mikondo ya kidato cha kwanza hadi cha nne ili kuhimiza matumizi ya TEHAMA.

“Nimefurahi kuona mna jengo maalumu la TEHAMA. Hii inaakisi malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka TEHAMA isambae nchi nzima.”

Amesema amefurahi pia kusikia Halmashauri hiyo ina lengo la kuifanya shule hiyo iwe na kidato cha tano na sita. “Mkurugenzi Mtendaji fanyeni maamuzi ili madarasa ya kidato cha tano na sita yajengwe na muweze kuwapa fursa watoto wa kike wa wilaya hii. Pia mtatoa chachu kwa  hawa wa kidato cha kwanza hadi nne ili wasome kwa bidii,” alisema.

About Author

Bongo News

4 Comments

    Dear [Recipient’s Name],

    I hope this message finds you well. I am writing to share an exciting opportunity to elevate the online presence and authority of [Their Website Name]. At [Your Company Name], we specialize in driving digital success through powerful backlink building strategies.

    Discover the Benefits:

    Boosted Rankings: Our proven methods will enhance your website’s search engine rankings.

    Increased Traffic: Enjoy a surge in organic traffic as your website gains more visibility.

    Enhanced Credibility: Quality backlinks from authoritative sources will elevate your site’s online credibility.

    Exclusive Offer:

    Explore our limited-time offer tailored just for you! Click [here](insert your website link) to uncover a world of possibilities for your website’s success. Our package includes:

    In-depth backlink analysis.
    Customized strategy development.
    Outreach to influential websites for premium link acquisition.
    Regular progress reports for transparency.
    Why Act Now:

    Seize this opportunity to propel your website to new heights! Click [here](insert your website link) to view our exclusive offer and take the first step toward digital excellence.

    We look forward to being a part of your website’s success story.

    Best regards,
    Aleksandar Djordjevic
    CEO of Wptechguys
    Wp Tech Guys
    wptechguys.com
    Visit: https://wptechguys.com/backlinkpro-building-bridges-to-digital-success/

    After study a few of the blog posts on your website now, and I truly like your way of blogging. I bookmarked it to my bookmark website list and will be checking back soon. Pls check out my web site as well and let me know what you think.

    Dear CEO,

    We are an investment and funding firm, working in alliance with a high-net-worth group to provide financing at minimal interest rates. We believe that a strategic partnership between our organizations could create substantial value for both parties.

    We would be delighted to share more details about this opportunity upon your response. Please feel free to reach out if you require any additional information or would like to discuss this further.

    Looking forward to your thoughts.

    Best regards,

    Art Allen

    Thank you for sharing your insights with the world. I really appreciate reading your website.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *