KITAIFA

WAZIRI MKUU AWAPA WATENDAJI TARURA, DAWASA SIKU 7 KUKAMILISHA BARABARA MUHIMBILI

WAZIRI MKUU AWAPA WATENDAJI TARURA, DAWASA SIKU 7  KUKAMILISHA BARABARA MUHIMBILI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usafi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA) Lydia Ndibalema wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia  barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo.

About Author

Bongo News

2 Comments

    I truly appreciate this post. I have been looking all over for this! Thank goodness I found it on Bing. You have made my day! Thx again

    Given a gene list, MOET identifies significantly overrepresented ontology terms using a hypergeometric test and provides nominal and Bonferroni adjusted P values priligy review

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *