Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango amesema serikali ya awamu ya sita ina dhamira ya dhati kuhakikisha
huduma bora za afya zinasogezwa Jirani na wananchi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za
mashine ya MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya iliogharimu shilingi
bilioni 3. Amesema kusogezwa kwa huduma bora kama uwepo wa MRI katika
hospitali hiyo ni lengo la kuwapunguzia wananchi gharama na adha za
kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.
Makamu wa Rais ameupongeza uongozi na wahudumu katika hospitali hiyo
kwa kuendelea kujitoa katika kuwahumia wananchi na ubunifu walioufanya
katika kutafuta vifaa mbalimbali ikiwemo vya kusafirisha wagonjwa ndani ya
hospitali.
Aidha ametoa wito kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya
kuzingatia utunzaji wa MRI hiyo ikiwemo kuzingatia muda maalumu wa
matengenezo uliopangwa ili itoe huduma kwa muda mrefu.
Pia ameagiza Wizara ya Afya kukamilisha utaratibu unaopaswa ili kuifanya
Hospitali hiyo kuwa taasisi na kujiendesha kiufanisi zaidi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema
wabunifu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wako katika hatua za
mwisho kutengeneza kifaa maalum kinachowekwa mkononi kwa mgonjwa
kitakachoweza kutuma ripoti kwa daktari muda wote hali ya hali ya mgonjwa
inavyobadilika hata akiwa mbali na hospitali.
Amewapongeza wabunifu katika hospitali hiyo kwa kutumia rasilimali ziliozopo
kubuni masuluhisho mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma bora hospitalini.
1 Comment
I would like to get across my love for your kind-heartedness supporting those people that should have guidance on in this idea. Your real dedication to getting the message all through had become wonderfully useful and have permitted regular people much like me to get to their aims. Your amazing helpful guidelines can mean a whole lot to me and additionally to my mates. Thank you; from everyone of us.