Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Mionzi la Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo
tarehe 22 Julai 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wahudumu wa
afya kwa kuhakikisha inaboresha Maisha yao na vitendea kazi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 22 Julai 2023 wakati akizindua
Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma akiwa katika siku ya
tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Ametoa wito kwa watoa huduma za
afya kutunza vifaa tiba ikiwemo kuweka utaratibu mzuri wa matengenezo ili
viweze kutoa huduma kwa wananchi wakati wote.
Makamu wa Rais amesema ni dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inasogeza huduma bora za afya karibu na
wananchi ikiwemo kupeleka vifaa tiba vya kisasa katika hospitali za mikoa ili
kuwapunguzia gharama wananchi kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali.
Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali inathamini mchango wa watoa
huduma za afya kwa kuwa wanamchango mkubwa katika kuwahudumia
wananchi na kuokoa Maisha yao. Amewasihi wahudumu wa afya kuendelea
kuwahudumia wananchi kwa upendo mkubwa.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaendelea na ziara ya kikazi mkoani
Ruvuma yenye lengo la Kusikiliza changamoto za wananchi, kukagua miradi
ya maendeleo pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akieleza juu ya
Mashine ya X- Ray ya Kisasa iliopo katika Hospitali ya Ruvaa ya Mkoa wa
Ruvuma wakati akikagua vifaa tiba vilivyopo katika Jengo la Mionzi la Hospitali
hiyo alipowasili kuzindua jengo hilo akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe
22 Julai 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu wa Afya wakati akikagua
vifaa tiba vilivyopo katika Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Ruvuma alipowasili kuzindua jengo hilo akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo
tarehe 22 Julai 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akivuta kitambaa kuweka jiwe la msingi la Uzinduzi wa Jengo la
Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua akiwa ziarani
mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango akihutubia wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Mwengemshindo mara
baada ya kuzindua Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma
alilozindua akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.