KITAIFA

MAKONDA AGEUKA MBOGO MULEBA” HAPA KUNA HARUFU YA RUSHWA, TAKUKURU LAZIMA WAFIKE HAPA

MAKONDA AGEUKA MBOGO MULEBA” HAPA KUNA HARUFU YA RUSHWA, TAKUKURU LAZIMA WAFIKE HAPA

Wakazi wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamepokea matumaini mapya kutoka kwa Katibu mkuu NEC , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Christian Makonda baada yakuwaahidi changamoto zinazowakabili sasa zimefika mwisho kwakua chama cha Mapinduzi kimerudi kwenye misingi yake.

Makonda wakati akihutubia wakazi wa eneo hilo leo November 10 ,2023 akiwa njiani kuelekea Chato amesema amipita hapo akiwa na mambo matatu likiwemo kumsapoti Mheshimiwa Rais,Suala la uwepo wa rushwa Muleba,Na changamoto ya Maji

“Mimi nina mambo matatu tu wana Muleba kwanza tumuunge mkono Dokta Samia kama kuna mahala hapaja enda sawa basi ni sisi wafanyakazi wake la pili ni rushwa kuna rushwa Kwenye ofisi za utumishi wa Umma , Kwenye vituo vya Polisi pia Maeneo mengi sana! na Kuhusu Changamoto ya maji nitaongea na waziri ahakikishe analeta vipi maji Muleba”CDE Makonda

Wakati huo huo ,Makonda ameongeza kuwa kuhusu suala la rushwa ataongea na Mkurugenzi mkuu mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) na itaundwa timu kuhakikisha kua changamoto hio sio sehemu ya wilaya Muleba

Hatahivyo Kwa upande wao Wakazi wa eneo hilo wameoneshwa kufurahishwa na uwepo wa kiongozi huyo katika nafasi yake Taifa na wamesema walitarajia muda zaidi kuwasilisha Kero kwake kwakua ameanza vizuri kazi yake

Mkazi mmoja aliyejiitambulisha mbele ya muandishi wa habari kwa jina la Mzee Magesa amesema mvua imewakatili walitaka wahoji zaidi kuhusu namna atakavyowasaidia na pengine kuwataja viongozi wanaowakwamisha lakini ameurahia uwepo wake hapo

“Hapa Tupo pembeni yake akiwepo yeye tunaona matumani kutokana na jinsi alivyoanza kazi kwenye kiti chake kipya Rais hajakosea tazama hapa mvua inanyesha lakini hata mimi nilitamani nihoji mengi zaidi kuhusu Muleba na wapo viongozi nawajua labda ije Takukuru kama alivyosema itatupa mwanga wa yeye kurudi tena hapa na tunamkaribisha” Mzee Magesa

Aidha , Ikumbukwe Katibu huyo yupo Kanda ya ziwa katika ziara ya kikazi ambayo ina malengo kadhaa ikiwemo kutatua na kusikiliza kero za wananchi .

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *