Uncategorized

MAKONDA AKUTANA NA MABALOZI OFISINI KWAKE, WAMPA MBINU ZA UTALII

MAKONDA AKUTANA NA MABALOZI OFISINI KWAKE, WAMPA MBINU ZA UTALII

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ameahidi kuendelea kutilia mkazo uimarishaji wa huduma za kijamii, usalama wa miundombinu mbalimbali ya Jiji la Arusha ili kuendelea kuifanya Arusha kuwa sehemu salama kwa watalii na wageni wanaodhuru Mkoani hapa kwa shughuli mbalimbali.

RC. Makonda ametoa kauli hiyo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani,  Balozi Hassan Idd Mwameta na Balozi Jestas Nyamanga, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji waliofika Ofisini kwake mapema leo kuzungumza naye kuhusu namna ya kustawisha sekta ya utalii mkoani Arusha.

Mabalozi hao wamemueleza RC. Makonda kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi wanazoiwakilisha Tanzania na kuahidi kumpatia ushirikiano mkubwa katika kutangaza na kuvutia watalii na wawekezaji kuja kutembelea na kutalii Mkoani Arusha.

Paul Makonda pia ameahidi kuendelea kuimarisha na kukuza uelewa wa wana Arusha katika kuuelewa Utalii na fursa za utalii zilizopo Arusha ili Kuendelea kuifanya Arusha kuwa Kitovu cha Utalii Barani Afrika.

Mkuu wa Mkoa ametumia fursa hiyo pia kuomba kuandaliwa kwa Mkutano maalum utakaohusisha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania kwenye Mataifa mbalimbali ili kupata uelewa wa kutosha kuhusu Mirejesho mbalimbali ya wageni na Raia wa kigeni wanaoitembelea Tanzania.

Kulingana na Mkuu wa Mkoa, Kikao cha Mabalozi hao kimekuwa kikao muhimu kwa ustawi wa Arusha kwani  amepata nafasi ya kupata uzoefu na uelewa zaidi kuhusu Utalii, Saikolojia ya wageni na mirejesho mbalimbali kutoka kwa Mabalozi hao kutoka kwa Wageni na watalii na wageni mbalimbali punde mara baada ya kurejea makwao wakitokea nchini Tanzania.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *