Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amesema wamejipanga kudhibiti magendo kwa kutumia Boti ya Doria iliyozinduliwa Ziwa Victoria.
Akizungumza jijini Mwanza baada ya uzinduzi wa Boti ya Doria ya TRA, Bw. Mwenda amesema Magendo yanayofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu yamekuwa yakichangia kuharibu Uchumi wa Nchi, kuhujumu Biashara za wengine, kuchochea uhalifu na kuharibu usalama wa Nchi, hivyo Boti ya Doria iliyozinduliwa itakomesha vitendo hivyo.
Amesema kuwa Boti ya Doria iliyozinduliwa itaokoa mapato yaliyokuwa yanapotea kutokana na ukwepaji kodi kupitia bidhaa za magendo.
“Miongoni mwa magendo makubwa yanayoingi kupitia Ziwa Victoria ni vipodozi ambavyo mbali na kukwepa kodi vimekuwa vikiharibu afya za wananchi na kazi yetu siyo tu kudhibiti tu mapato, pia tunaangalia afya za watanzania” Amesema Mwenda.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema walipakodi wa Tanzania wanataka kuwepo na usawa katika kodi hivyo kuzinduliwa kwa Boti hiyo kunatekeleza matakwa ya wananchi maana kwa kuzuia magendo kutakuwa na usawa wa biashara kwa kila mtu kulipa kodi.
“Usawa wa biashara unakosekana maana unakuta mtu aliyeingiza bidhaa za magendo anaziuza kwa bei ya chini kuliko wenzake maana hajazilipia kodi, sasa tutahakikisha wote wanalipa kodi” Bw. Mwenda
Kamishna Mkuu Mwenda amesema Magendo yanayofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu yamekuwa yakichangia kuharibu Uchumi wa Nchi, kuhujumu Biashara za wengine, kuchochea uhalifu na kuharibu usalama wa Nchi, hivyo Boti ya Doria iliyozinduliwa leo mkoani Mwanza itakomesha vitendo hivyo.
Ameeleza kuwa TRA itatoa motisha kwa mwananchi yeyote atakayefichua watu wanaojihusisha na magendo au wanaokwepa kodi na kuwa suala la kotisha lipo kisheria.