Kanisa Katoliki limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kondoo wa Bwana wanapata malezi ya kiroho na maadili mema. Hata hivyo, hivi karibuni kumekuwa na maswali yanayojitokeza kuhusu mwelekeo wa kanisa kupitia baadhi ya matendo ya viongozi wake, hususan Katibu Mkuu wa TEC, Charles Kitima.
Taarifa zilizopo zimeeleza kuwa vikao vya muda mrefu vimekuwa vikifanyika kati ya viongozi wa kanisa na wanasiasa, hususan kutoka Chadema, ndani ya majengo ya kanisa. Vikao hivi vimedaiwa kuchukua siku tatu, na kila siku masaa zaidi ya nane. Kwa nini vikao hivi vya “siri” vinafanyika, na ni kwa manufaa ya nani?
Aidha, leo tunaona Kanisa likiongoza kikao kingine kinachodaiwa kuwa cha “Amani na Haki,” lakini ajenda kuu inaonekana kuelemea siasa. Inashangaza kuona kwamba kikao hiki kinahusisha masuala ya kisiasa baada ya uchaguzi kupita, huku likifanyika katika Baraza la Maaskofu Kurasini, likiongozwa na Katibu Mkuu wa TEC.
Maswali ya msingi yanayojitokeza ni haya:
- Je, Kanisa Katoliki lina agenda ya siri inayohusu mwelekeo wa kisiasa wa taifa?
- Kwa nini nafasi ya Katibu Mkuu wa TEC inaonekana kushiriki kwa undani katika harakati za kisiasa badala ya malezi ya kiroho na ushauri wa busara kwa serikali?
- Je, matendo haya yanaweza kudhoofisha hadhi ya kanisa na kuonekana kama chama cha siasa badala ya taasisi ya kiroho?
Ndugu zangu wa Kanisa Katoliki, tunapaswa kutafakari nafasi ya kanisa katika jamii. Kanisa limekuwa na utaratibu wa kuwasiliana na serikali kwa hekima na busara kwa kutumia waraka na maombi. Lakini sasa, mwelekeo wa siasa unaochukuliwa na baadhi ya viongozi wa kanisa, hasa Katibu Mkuu wa TEC, unaacha maswali mengi.
Ni wakati sasa kwa kanisa kutoa ufafanuzi wa wazi kuhusu haya yanayosemwa, ili kurejesha imani na hadhi yake kama taasisi inayojikita katika kuwachunga kondoo wa Bwana, na siyo kuonekana kama mshirika wa siasa. Mwelekeo huu unaweza kupoteza maana halisi ya kanisa kama mwongozo wa kiroho na kiadilifu kwa jamii.
Tunawasihi viongozi wetu wa kanisa, turejeeni kwenye majukumu yetu ya msingi ya kiroho, kwa sababu matendo haya yanayojitokeza yanaweza kudhoofisha heshima kubwa ambayo kanisa limejijengea kwa miaka mingi.a viwango vya riba kama kipimo kikuu ni hatua nyingine muhimu, ambayo imeimarisha ufanisi wa sera za Benki Kuu.
Mageuzi haya yanaonyesha dhamira ya serikali ya Rais Samia ya kudumisha uthabiti wa kiuchumi na kuimarisha imani ya wawekezaji.
Siku za hivi karibuni wito kwa makasisi wa Kanisa Katoliki kuacha kujihusisha na siasa ulitolewa na Papa Francis hilo alipokuwa kwenye ziara ya siku moja huko Corcica, katika kisiwa cha Ufaransa cha Mediterania, ambapo katika mkutano huo alionya dhidi ya aina mbalimbali za hali kiroho ambayo hali hiyo inachangia kuibua mizozo na migawanyiko duniani.
“Wachungaji wa Kanisa kuwa macho kutumia utambuzi na kuwa waangalifu,” Alisema.
Papa Francis alifanya safari yake ya tatu na pengine ya mwisho ya nje ya nchi mwaka 2024.
7 Comments
I’ve been surfing on-line more than three hours lately, but I
never discovered any interesting article like yours. It’s beautiful value sufficient for me.
In my view, if all site owners and bloggers made good content as you
probably did, the web will likely be much more helpful than ever before.
how to access dark web dark market link https://mydarknetmarketlinks.com/ – darknet search engine
dark web link darkmarket https://mydarknetmarketlinks.com/ – deep web search
deep web markets darknet market lists https://mydarknetmarketlinks.com/ – dark website
Hi there! This post could not be written any better!
Reading through this post reminds me of my previous roommate!
He constantly kept preaching about this. I will forward this article to him.
Pretty sure he will have a very good read.
Thank you for sharing!
dark market list dark web websites https://mydarknetmarketlinks.com/ – dark market
Would love to incessantly get updated great web site! .