SHULE za FEZA (FEZA SCHOOLS) zinajivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi kuwa bora na ndio siri ya kufanya vizuri kila mwaka katika mitihani ya Taifa ambapo imeendelea kung’ara baada ya wanafunzi wao wote waliofanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka jana kupata daraja la kwanza(div I), huku asilimia zaidi ya 65 wakipata div 1.7.
Hayo yamesema na Makamu Mkuu wa Shule ya FEZA Wavulana, Shabani Mbonde wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2024 katika shule hiyo iliyopo Kunduchi Dar es Salaam mara baada ya Baraza la Mitihani kutangaza matokeo ya kidato cha nne.
Mbone ameleeza kuwa matokeo hayo hajatokea tu kirahisi bali ni uwekezaji na mazingira ya shule yanayomtengeza mwanafunzi kuwa bora na walimu wa kutosha ambapo kila mwalimu ana wastani ya kufundisha wanafunzi 10.
” FEZA SHOOLS haitoi mwanafunzi bora katika A tu, bali katika nyanja zote.Sisi katika elimu hatumjengi mwanafunzi kupata A tu lakini pia katika kukabiliana na hali zote katika maisha kulingana na wakati uliopo.
“Hii yote inatokana na jitihada mbalimbali za wanafunzi wenyewe na walimu. Mwanafunzi wetu anakuwa ni kama ametoka kwenye mashine au kiwanda kilichomjenga katika kupambana na changamoto mbalimbali katika mtihani na maisha.Tunajivunia wanafunzi wetu na walimu wetu,” amesema Makamu Mkuu huyo.
Aidha Mbonde amesema kama sekta binafsi wanashukuru serikali kwa kusisitiza suala la elimu na wanaiunga mkono Serikali katika kuhakikisha elimu inakuwa bora.
Naye Mkuu wa taaluma msaidizi wankidato cha tatu na nne, Abdallah Juma ameeleza mbinu wanazotumia kuwafundisha wanafunzi hao kuwa ni progamu mbalimbali walizonazo shuleni hapo.
” Sio kwamba sisi vijana wote tunaowachukua ni wale ‘cream’ tu bali wanakuja hata wenye uwezo mdogo tunawatengeneza na wanakiwa sawa na wenzao na wanafaulu kwa pamoja.
” Matokeo haya yamepatikana kwa njia tofauti, pande zote tatu zina mchango yaani wazazi, walimu na wanafunzi, pia tuna programu mbalimbali za masomo kuanzia asubuhi, jioni na hata usiku, pia wanapata muda wa kucheza”, amesema.
Kwa upande mmoja wa wanafunzi wa FEZA BOYS waliofanya vizuri kwa kupata division one 1.7, Moses Francis, amesema anamshukuru Mungu kwani mafanikio hayo hayakuja kirahisi ya kupata A masomo yote 10 ila mazingira ya shule yamechangia ikiwamo kusoma kwa bidii kama mwanafunzi.
Amefafanua kuwa kutokana na ratiba za shule zilivyopangiliwa wanapata muda wa kutosha wa kupumzika lakini kuna kipindi kigumu unatakiwa kusoma sana ili kufaulu mtihani.
“Hii haipatikani kirahisi, mtu kufaulu lazima kuwe na motisha kuanzia kwa mwanafunzi wenyewe na mzingira mazuri ya kujifunzia pamoja na kumtanguliza Mungu.Kila wiki tunafanya mazoezi ya masomo kwa kufanya test,” amesema Moses.
Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ufaulu umeongezeka ambapo jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo sawa na asilimia 92.32 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I,II,III,IV
7 Comments
If you are going for best contents like myself, simply go to see
this web page every day since it offers feature contents, thanks
X poker официальный сайт
If some one needs expert view on the topic of
blogging and site-building after that i advise him/her to pay a
quick visit this web site, Keep up the fastidious work.
х покер без регистрации
X poker с минимальным депозитом
pppoker live games
РРєСЃ покер регистрация