KITAIFA

MAVUNDE AIPONGEZA STAMICO KWA KUPIGA HATUA NA KUJITEGEMEA

MAVUNDE AIPONGEZA STAMICO KWA KUPIGA HATUA NA KUJITEGEMEA

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa hatua kubwa iliyopigwa katika kipindi kifupi  kutoka kuwa Shirika tegemezi na kuwa Shirika linalojitegemea huku akilitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufikia azma ya kuwepo kwa Shirika hilo.

Aliyasema hayo Septemba 05, 2023 jijini Dodoma katika kikao kifupi  na Menejimenti ya Shirika hilo ambapo alieleza kuwa STAMICO imefanya kazi kubwa sana katika muda mfupi na kuleta ushindani  dhidi ya kampuni kubwa zilizokuwa zimezoeleka katika Sekta ya Madini hapa nchini.

Waziri Mavunde alisema kuwa Shirika hilo limeonesha kuwa hakuna jambo linaloshindikana; kujitolea, uadilifu na maono ni chachu iliyopelekea mafanikio katika Shirika hilo.

“lakini nimpongeze Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Venance Mwasse tangu amefika hapa amefanya mapinduzi makubwa lakini bila ninyi asingeweza peke yake, nawapongeza sana na hiki kiwe kichocheo cha kufanya vizuri zaidi” alisema Mhe. Mavunde.

“Lakini kwa upekee sana nimpongeze Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara, Kheri Mahimbali kwa usimamizi wao thabiti bila wao yawezekana msingefika hapa na nyinyi wenyewe mmekiri kuwa Wizara imewasaidia sana kufanya mapinduzi haya makubwa” aliongeza Mhe. Mavunde.

Aidha, aliitaka Shirika hilo kufikiria kufanya kazi zaidi hadi nje ya mipaka ili kujiimarisha na kujitangaza zaidi kwa kuleta ushindani katika tasnia ikiwemo ya Uchorongaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo alimpongeza Mhe.Mavunde kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Madini na kumuahidi kuwa Shirika litafanyia kazi maelekezo yake ili kufikia lengo.

Akizungumzia Mipango ya Shirika hilo, Meneja Rasilimali Watu Deusdedith  Magala alieeleza kuwa  Shirika limepanga kuondokana kabisa na utegemezi wa mishahara kutoka serikalini  kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025; kuongeza gawio lake serikalini mwaka 2024/2025; kuzalisha kwa wingi Mkaa mbadal

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *