Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kudumu wa Kamati ya Bunge Elimu Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko, amewawezesha wanawake zaidi ya 800 kutoka wilaya tisa za Mkoa wa Tanga kupata mafunzo ya ujasiriamali.
Mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Husna Sekiboko na kufanyika wilayani Korogwe, yamelenga kuwasaidia wanawake kufikia maendeleo kupitia biashara zao ndogondogo.
Nimeamua kuwezesha mafunzo haya kwa wanawake kutoka wilaya tisa za mkoa wa Tanga sababu nimeona kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya ujasiriamali katika ngazi za vijiji na kata” Alisisitiza Sekiboko
Hata hivyo alisema anamshukuru Rais Samia kwa kuamua kurudisha mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake vijana na watu wenye ulemavu ndo maana nimeamua kutafuta wataalam wa ujasiriamali ili wasasaidie kujua matumizi ya fedha hizo lakini pia mjue na namna ya kurejesha