Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Lembrus Mchome, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari leo saa 5 asubuhi, jijini Arusha.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utatoa picha ya kinachoendelea katika chama chake, ukiwepo mpango wa kufukuzwa na viongozi wa juu wa chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa chama hicho uliofanywa katika Uchaguzi Mkuu sanjari na uteuzi wa viongozi watano wa Kamati Kuu wa Chadema.

imeelezwa kuwa Mchome anatoka hadharani kuzungumzia jinsi viongozi hao wa Chadema, chini ya Mwenyekiti wa Taifa Tundu Lissu na Makamu wake John Heche, walivyoamua kusigina Katiba yao, huku wakikataa kukosolewa na wanachama wanaotofautiana kimtazamo.

Lissu na viongozi wenzake wa Chadema wanadaiwa kuwa wamejinasibu kama moja ya watu wanaopenda kuikosoa serikali, licha ya wao kushindwa kuvumilia wanapokosolewa katika uendeshaji wa chama chao.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *